
Katika kuadhimisha kilele cha Siku ya Haki za Binadamu duniani, leo Shirika la Global Peace Tanzania ikishirikiana na Washiriki wao Youth of United Nations (Yuna) Tanzania wameendesha Mjadala juu ya siku 16 za kupinga Ukatili wa Kijinsia, mjadala ulijikita zaidi katika kujadili haki za Watu wenye ulemavu Tanzania.
Sherehe hizi zilifanyikia katika ukumbi wa mkutano wa ofisi za Umoja wa Mataifa, Masaki Dar Es Salaam, Tanzania Mgeni rasmi alikuwa Bi Ummy Nderiananga Mwenyekiti wa Chama Cha Walemavu Tanzania SHIVYAWATA)

Mgeni rasmi Bi Ummy Nderiananga Mwenyekiti wa Chama cha walemavu Tanzania, akielezea changamoto mbalimbali zinazowakabili watu wenye ulemavu .Mgeni maalumu Ndugu Stella Swaumu Vuzo, Afisa habari Umoja wa Mataifa akielezea kwa kirefu historia ya siku ya haki za binadamu na umuhimu wa kuadhimisha siku hii maalumu.


Washiriki walipata nafasi ya kujadili kwa undani juu ya Haki za Binadamu, hususani haki za watu wenye ulemavu, aidha washiriki wamesisitizia uwepo wa mazingira rafiki ya kuwahudumia watu wenye ulemavu wanaopitia masuala ya ukatili wa kijinsia
Leo tumeadhimisha kilele cha Siku ya Haki za Binadamu, lakini harakati hizi bado zinaendelea, ni za kila siku mpaka pale Ukatili wa kijinsia utakapo tokomezwa.
#16DaysofActivism#HumanRightsDay#LeavingNoOneBehind#OrangeTheWorld#Tanzania #GlobalPeace #UN
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...