Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini IGP Simon Sirro ameendelea kuwaonya watu wanaonyanyasa wanawake na watoto, kwa kuwasababisia vipigo na ukatili wa aina nyingine ambao ni kinyume cha sheria za nchi.
IGP Sirro amesema hayo leo wakati akizindua Ofisi za Dawati la Jinsia na Watoto wilayani Bunda mkoani Mara, ujenzi uliofadhiliwa na Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Idadi ya Watu Duniani UNFPA pamoja na Shirika la Jukwaa la Utu wa Mtoto yaani CDF.
Katika sherehe hizo za uzinduzi IGP Sirro amewataka wananchi kutumia ofisi hiyo ya Dawati la kijinsia na watoto ili kuendelea kukomesha vitendo vya ukatili sambamba na kuwataka wazazi kuwaendeleza kielimu watoto wao jambo ambalo litasaidia jamii kuwa na viongozi bora.
Naye Mkuu wa Wilaya ya Bunda Mhe. Lydia Bupilipili amesema kuwa, Jeshi la Polisi limeweza kuchukua hatua madhubuti hususani katika kudhibiti vitendo vya unyanyasaji wa kijinsia, ukatili, mimba za utotoni, ulawiti, na ubakaji
Aidha, katika ziara yake mkoani Mara, IGP Sirro tayari amekwisha zindua jumla ya Ofisi nne za Dawati la Jinsia na Watoto hatua ambayo itarahisisha upatikanaji wa taarifa zinazoripotiwa kwenye madawati hayo kuhusiana na masuala ya unyanyasaji wa kijinsia.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...