Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini IGP Simon Sirro
KIBAHA, PWANI
Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini IGP Simon Sirro amewataka wananchi kote nchini kuendelea kuitunza na kuimarisha hali ya amani na usalama nchini na kujiepusha kushiriki katika vitendo vya kihalifu.
IGP Sirro amesema hayo leo Kibaha mkoani Pwani akikagua mradi wa nyumba 24 za makazi ya askari Polisi na familia zao, ambapo amewaagiza Makamanda wa Polisi kote nchini kuimarisha doria na misako ili kuhakikisha Watanzania wanasherehekea sikukuu kwa amani huku wale watakao vunja amani ya nchi kushughulikiwa kwa mujibu wa sheria.
Hata hivyo, akikagua nyumba za makazi ya askari Polisi IGP Sirro ameendelea kumpongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Magufuli, kwa kuunga mkono jitihada zinazofanywa na Jeshi hilo.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...