Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Mhe.
Daniel Chongolo akiangalia mtambo wa kuchakata kokoto katika ujenzi wa
kituo cha Afya cha Makumbusho, walipokuwa na wajumbe wa kamati ya siasa
ya CCM Wilaya.

Muonekano wa mradi wa ujenzi wa Zahanati ya Magomeni ambapo wajumbe wa kamati ya siasa ya Wilaya wakikagua mradi huo.

Muonekano wa Kituo cha Afya cha Kigogo ambapo wa jumbe wa kamati ya siasa ya Wilaya ya Kinondoni walifanya ziara hap jana.

Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya
Kinondoni, Harlod Maruma, akiwa na Mbunge wa jimbo hilo Maulid Mtulia
mwnye tisheti ya njano, akiwa na wajumbe wa kamati hiyo walipokuwa
katika mradi wa ujenzi wa kituo cha Afya cha Makumbusho.

Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya
Kinondoni, Harlod Maruma, mwenye miwani akiwa na wajumbe wa kamati hiyo
walipokuwa wakikagua mradi wa ujenzi wa Zahanati ya Makumbusho.
Mweyeshati jeupe ni Mkuu wa Wilaya hiyo Mhe. Daniel Chongolo.

Katibu wa Chama Cha Mapinduzi CCM
Wilaya ya Kinondoni, Sure Mwasanguti wa kwanza kulia akimueleza jambo
Mkuu wa Wilaya hiyo Mhe. Daniel Chongolo ,wakati wa ukaguzi wa miradi
mbalimbali ya Halmashauri hiyo, katikati mwenyemiwani ni Mwenyekiti wa
Jumuiya ya wazazi CCM Wilaya , Said subety .
*****************************************
Kamati ya siasa ya Chama Cha
Mapinduzi CCM Wilaya ya Kinondoni jana imefanya ziara ya kutembelea na
kukagua miradi sita iliyopo katika Kata tano kati ya kata 20 zilizopo
katika Halmashauri hiyo.
Ziara hiyo ambayo ilikuwa
ikiongozwa na Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Wilaya Harlod
Maruma, ilihusisha viongozi wengine akiwemo Mkuu wa Wilaya hiyo Mhe.
Daniel Chongolo, Mstahiki Meya Benjamini Sita, Kaimu Mkurugenzi wa
Halmashauri hiyo Dk. Patricia Henjewele, Mbunge wa jimbo hilo Maulid
Mtulia, watendaji pamoja na wakuu wa Idara mbalimbali.
Aidha kamati hiyo ilitembelea
mradi wa Kituo Cha Afya Cha Kigogo kinachojengwa kwa shingili milioni
700 ambapo kati ya fedha hizo shilingi milioni 400 ni pesa kutoka
Serikali kuu, shilingi milioni 300 ni pesa zinazotokana na mapato ya
ndani ya Halmashauri.
Kamati hiyo ilitembelea mradi
mkubwa wa Soko la Kisasa la Magomeni linalojengwa kwa shilingi Bilioni
8.9 ambapo kamati hiyo ilieleza kuwa imeridhishwa na hatua ya soko hilo
ilipofikia kwa sasa na hivyo kutumia nafasi hiyo kumpongeza Mkurugenzi
Ndugu. Aron Kagurumjuli na watendaji wake.
Kamati hiyo pia ilitembelea mradi
wa ujenzi wa vyumba sita vya madarasa ya ghorofa shule ya Sekondari
Mzimuni, ambapo Mkuu wa shule hiyo , Yahaya Kirondo alisema kuwa
kulingana na kasi ya ujenzi unavyo endelea hadi kufikia Januari 2020
wanafunzi waliochaguliwa kujiunga na kidato cha kwanza katika shule hiyo
wataanza kutumia madarasa hayo.
Aidha kamati hiyo pia ilitembelea
ujenzi wa Zahanati ya Magomeni, Makumbusho ambapo kwa mujibu wa
mkandarasi mshauri anayesimamia ujenzi wa Zahanati hizo, alisema kuwa
hadi kufikia Aprili 2020 zitakuwa zimekamilika na hivyo wananchi kuanza
kupata huduma.
Mkuu wa Wilaya hiyo, Mhe. Daniel
Chongolo aliieleza kamati hiyo kuwa, kumalizika kwa Zahanati hizo
kutasaidia kuwa rahisishia wananchi kupata huduma za karibu katika
Zahanati hizo badala ya kwenda moja kwa moja katika Kituo Cha Afya cha
Magomeni au Hospital ya Rufaa ya Mwananyamala.
Mhe. Chongolo alisema kuwa,
Zahanati hizo pia zitakuwa msaada mkubwa kwa wananchi wa Magomeni na
maeneo mengine kwa kuwa eneo hilo linawakazi wengi na kwamba ha kukuwa
na Zahanati zaidi ya Hospitali ya Rufaa ya Mwananyamala na Kituo cha
Afya Cha Magomeni.
Miradi mingine iliyotembelewa na
kamati hiyo ni ujenzi wa barabara zinazo simamiwa na DMDP ambazo ni
Shekilango yenye urefu wa kilomita 3.7, Barabara ya Akachube yenye urefu
wa kilomita 0.94, barabaa ya TRA yenye urefu wa kilomia 1.1, barabara
ya Sinza Mori yenye urefu wa kilomita 0.93 na Igesa yenye urefu wa
kilomita 0.64.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...