TAALUMA ya ustawi wa jamii imekua ni tegemeo la nchi zote hapa Duniani, Kwa nyakati tofauti kwani Kumekua na Sheria na taratibu zilizowekwa na kila nchi, msingi wake mkubwa ni kulinda jamii zao dhidi ya unyanyasaji wa aina yoyote na kuleta ustawi kwenye jamii.

Hayo yamesemw na Naibu Waziri wa Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Josephat Kandege (MB) wakati akizungumza na wahitimu wa Taasisi ya Usitawi wa jamii katika mahafali ya 43 ya Taasisi hiyo jijini Dar es Salaam leo. Amesema kuwa baadhi ya nchi za Ulaya na Amerika  wamekua na sheria kali na madhubuti katika kukabiliana na unyanyasaji wa aina yoyote hasa kwenye makundi athirika  hususani wanawake na watoto. 

Kandege amesema kuwa Taaluma ya Ustawi wa Jamii ni taaluma muhimu sana na inayohitaji weledi wa hali ya juu wahiti waliofanikiwa kuhitimisha masomo yao leo wajione na dhamani kubwa kwani umhimu wa watu hao katika jamii ni mkubwa.

"Taaluma hii imeleta mapinduzi ya kiuchumi ikiwemo mapinduzi ya viwanda katika nchi mbalimbali kama Norway, Denmark na nchi nyinginezo za ‘Scandinavia’". Amesema Kandege.

Hata hivyo Kandege amesema kuwa hapa nchini tunasheria zinazolenga kuwalinda wahanga kwa kiasi kikubwa cha unyanyasaji katika jamii zetu, hasa Wanawake na Watoto, Watu wenye Ulemavu pamoja na Kundi la Wazee. 

"Pamoja na kuwepo kwa Sheria hizo bado tunazo changamoto kubwa ndani ya jamii yetu na kwa kiasi kikubwa ipo haja ya Wataalam wa Ustawi wa Jamii kuongeza kasi katika kusimamia utekelezaji wa sheria hizo".

Changamoto kubwa iliyopo ni ongezeko  la watoto wa mitaani, ubakaji kwa watoto, watoto wa shule kupewa mimba, kushuka kwa maadili ndani ya jamii yetu, kuzorota kwa malezi na makuzi kwa watoto, uhafifu wa matunzo kwa wazee kutoka kwa jamii ,ongezeko la Ulevi wa kupindukia kwa vijana, kubaguliwa kwa  watu wenye ulemavu na ongezeko la matumizi mabaya ya mtandao wa intaneti kwa kundi la vijana. 

Kwa Upande wake Mkuu wa Taasisi ya Ustawi wa Jamii, Dkt. Joyce Nyoni amewapongeza wahitimu wote pamoja na kuwashukuru wazazi, walezi, ndugu, jamaa na marafiki kwa kuwezesha kwa namna  moja au nyingine wahitimu kufikia hatuamuhimu waliofikia.

Pia amesema kuwa watafanya kazi kwa bidii ili kuweza kufikia malengo yaliyopangwa na serikali.

"tunaahidi kwamba tutafanya kazi kwa bidi na nguvu zetu zote ili kuhakikisha tunafikia malengo yaliyopangwa na kuendelea kuwa na mchango mkubwa katika kuleta maendeleo ya kiuchumi na kijamii nchini na tunaahidi hatutakuangusha. "
 Naibu Waziri wa Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Josephat Kandege (MB) akizungumza na wahitimu pamoja na wakufunzi na wageni mbalimbali waliohudhulia mahafali ya 43 ya Taasisi ya Ustawi wa Jamii jiji ni Dar es Salaam leo.

Mkuu wa Taasisi ya Ustawi wa Jamii, Dkt. Joyce Nyoni  akizungumza wakati wa Mahafali ya 43 ya Taasisi ya Ustawi wa Jamii leo jijini Dar es Salaam.

Faudhia kitenge mmoja wa Wahitimu aliyefanya vizuri kwenye masomo akipokea cheti kutoka kwa Mgeni rasmi Naibu Waziri wa Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Josephat Kandege (MB). Leo katika Mahafali ya 43 ya Taasisi ya Usitawi wa Jamii jijini Dar es Salaam. 
 Wahitimu wakimsikiliza Mgeni Rasmi.
 Rais mstaafu wa Serikali ya wanafunzi wa Taasisi ya Usitawi wa Jamii, Raphael Mollel akipitia kitabu cha mahafali ya taasisi hiyo jijini Dar es Salaam leo.
 Wahitimu wakiwa katika pozi.

Wahitimu wa Mahafali ya 43 ya Taasisi ya Usitawi wa Jamii wakivaa kofia ikiwa ni ishara ya kutunukiwa shahada zao jijini Dar es Salaam leo.
Wahitimu.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...