Naibu Mkurugenzi Mtendaji wa MNH-Mloganzila, Dkt. Julieth Magandi
akikabidhiwa hati ya msaada wenye thamani ya milioni 10 uliotolewa na Benki ya NMB PLC, kulia ni Meneja wa Benki hiyo Tawi la Kibaha Bw. Hosea Lyatuu.
Mkuu wa Idara ya Huduma za Ukunga, Afya ya Uzazi Mama na Mtoto MNH-
Mloganzila Bi. Christina Mwandalima (kushoto) akiishukuru NMB kwa msaada huo, katikati ni Mkurugenzi wa Huduma za Tiba Dkt. Mohamed Mohamed.
Bw. Hosea Lyatuu (wa pili kulia) akizungumza na uongozi wa Hospitali ya
Mloganzila wakati akikabidhi msaada kwa niaba ya Benki ya NMB.
Baadhi ya viongozi wa MNH-Mloganzila wakiwa katika picha ya pamoja na
wafanyakazi wa NMB mara baada ya kukabidhiwa msaada.
Vitanda 10, magodoro 10 na strecha mbili zilizokabidhiwa hospitalini hapa naBenki ya NMB.

*********************************

Hospitali ya Taifa Muhimbili-Mloganzila imepokea msaada kutoka Benki ya NMBwenye thamani ya Tsh. Milioni 10 ambao unalenga kuunga mkono juhudi zaserikali za kuboresha huduma za afya nchini.

Akikabidhi msaada kwa niaba ya Benki ya NMB PLC, Meneja wa Benki hiyo tawila Kibaha, Bw. Hosea Lyatuu ametaja msaada huo ni vitanda 10, magodoro 10pamoja na strecha mbili ambapo ameeleza kuwa NMB imekuwa ikitoa misaadakatika sekta tatu ikiwemo elimu na afya kwa lengo la kuisaidia jamii.

“Tumeamua kutoa msaada huu katika hospitali ya Mloganzila ili kuhakikisha kuwa kuna vitanda vya kutosha kwa ajili ya kutoa huduma za afya na benki yetu hufanya hivi ikiwa ni sehemu ya kurudisha fadhila kwa jamii,” amesema Bw. Lyatuu.

Bw. Lyatuu amefafanua kuwa wanatambua mchango unaotolewa na watoa
huduma za afya hivyo wameamua kutoa msaada katika sekta hii ili kuhakikishajamii inapata huduma pasipo shida yoyote.

Kwa upande wake Naibu Mkurugenzi Mtendaji wa MNH-Mloganzila, Dkt. Julieth Magandi ameishukuru Benki ya NMB kwa msaada huo ambao utaongeza idadi ya vitanda vitakavyotumika kwa ajili ya kutolea huduma hospitalini hapa.

“Tunawashukuru kwa msaada huu kwani umekuja wakati muafaka wakati hospitali hii inajikia katika kuanzisha huduma mpya hivyo tunatumaini NMB mtaendelea na juhudi hizi kwani hospitali yetu bado inahitaji msaada wenu kwa lengo la kuhudumia jamii,” amesema Dkt. Magandi.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...