Na. Irene Mwidima, Michuzi TV
MSANII wa bongo fleva Nuh Mziwanda amedai ya kwamba kati ya vitu anavyojutia kwenye maisha yake ni kuoa mapema. Nuh amesema alimuoa mke wake wa Kwanza Nawal Masoud kwa shinikizo la wazazi wa upande wa mwanamke baada ya wazazi wake kugundua kwamba mtoto wao ana ujauzito wake.
"Kwa kipindi chote Nawal alikuwa bado na umri mdogo wa miaka kumi na sita (16) tu, hivyo ilinilazimu kumuoa bila kujiandaa japo nilikuwa nikimpenda ila sikuwa na mipango ya kumuoa kwa kipindi hicho," Hata hivyo Mziwanda ameweka bayana kuwa kwa sasa hana Mahusiano na Nawal Kila mtu anaendelea na maisha yake.
"Nimeachana na mzazi mwenzangu Nawal bila hata ya talaka imetokea tuu mtu aliondoka na kwenda kwao na kisha nikasikia ameolewa tena hivyo yupo na maisha yake na mimi nipo na maisha yangu sikujisumbua kupeleka talaka maana amejipatia mwenyewe bila kosa lolote".
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...