Na Bakari Madjeshi, Michuzi TV

Droo ya Raundi ya Tatu ya Michuano ya Kombe la Shirikisho la Azam Sports (ASFC) imeendeshwa leo jijini Dar es Salaam, ikihusisha timu 64: Timu 20 kutoka Ligi Kuu, Timu 24 kutoka Ligi Daraja la kwanza na timu 20 zilizofuzu kutoka madaraja ya chini.

Katika Droo hiyo, timu ya Azam FC ya jijini Dar es Salaam ambao ndio Mabingwa Watetezi wa Michuano hiyo, Azam FC  watakumbana na timu ya African Lyon ya Dar es Salaam. Simba SC yenyewe itavaana na Arusha FC ya Arusha wakati Watani wao wa Jadi, Yanga SC watavaana na Iringa United ya Iringa.

Timu kutoka Tanga (Tanga Derby), Coastal Union ya mjini humo yenyewe itacheza na African Sports, mchezo utakaopigwa katika dimba la CCM Mkwakwani ikiwa ni Raundi hiyo ya Tatu ya Kombe ya Shirikisho (ASFC).

Timu nyingine za Ligi Kuu Soka Tanzania Bara ambazo zipo juu katika Msimamo wa Ligi hiyo ni Lipuli FC ya Iringa wataikaribisha Dar City ya Dar es Salaam, Kagera Sugar katika dimba la Kaitaba Stadium watacheza na Rufiji United, Tanzania Prisons wakiwa katika Dimba la Sokoine wataikaribisha Mlale FC.

Mtibwa Sugar wakiwa nyumbani Morogoro wataikaribisha Rhino Rangers, Namungo FC wakiwa katika dimba la Majaliwa Stadium watacheza na Green Warriors na JKT Tanzania watapepetana na Boma FC ya Mbeya.

Timu nyingine za Ligi Kuu ni Mbeya City dhidi ya Migombani, Polisi Tanzania watacheza dhidi ya Top Boys, Mwadui ya Shinyanga watacheza dhidi ya Mkamba Rangers ya Morogoro na Singida United itakuwa ugegeni kukabiliana na Tukuyu Stars ya Mbeya katika dimba la Uwanja wa Sokoine jijini Mbeya. 


Michezo mingine ni:-
KMC v Mbuni FC
Alliance FC  VS Transit CAMP
Ndanda FC VS Cosmopolitan
Ruvu Shooting VS Milambo FC
Mbao FC VS Stand UNITED
Biashara United VS Nyamongo

Mawenzi FC VS Mtwivila City
Mpwapwa VS Kitayosa
Friends Rangers VS Talinega FC
Kasulu Red Star VS Ihefu FC
Gipco VS Toto Africans
The Mighty Elephant VS Mashujaa FC
Jeshi Warriors VS Dodoma FC
Majimaji VS Pamba FC
Area C United VS Panama FC
Gwambina FC VS Mbeya Kwanza
Geita Gold VS Pan African
Sahare All Stars VS Njombe Mji

Mkurugenzi wa Mashindano wa Shrikisho la Soka nchini (TFF), Salum Madadi amesema mchakato wa sehemu ambapo itachezwa Fainali bado unaendelea, amesema michezo ya Raundi hiyo ya Tatu ya Michuano hiyo itaanza kucheza Desemba 22 na 23, 2019.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...