TAASISI ya Teknolojia Dar es Salaam (DIT) imeahidi kuisaidia Shule ya Kijeshi ya Ulinzi wa Anga Tanga (SKUA) kuandaa mtaala wa uhandisi umeme moja na masuala ya rada katika shule hiyo.

Kaimu Mkuu wa Chuo Taaluma na Mafunzo, Dk Ezekiel  Amri aliwaeleza timu ya wakufunzi walifika DIT jana kuwa ujumbe huo umekuja sehemu sahihi kwani DIT wamebobea katika katika sekta hiyo.

"Nataka niwahakikishie kwamba mlipokuja kupata msaada ni sehemu sahihi kabisa na sisi tunaahidi kuwasaidia ili muweze kufanikiwa katika hilo. DIT kwa hapa nchini tumebobea hasa na mitaala yetu ni bora," alisema Dk Ezekiel.

Naye Mkuu wa Mradi wa Kituo Cha Umahiri wa Tehama Cha Kikanda kijulikanacho kama RAFIC katika mradi wa EASTRIP, Joseph Matiko alisema kuwa fedha za mradi huo zinaweza kukisaidia chuo hicho cha Kijeshi kupata mtaala wake.

"Kwa upande wa mradi Mimi nitawasikisha hilo ili muweze kupata msaada wa fedha, pia mnaweza kusema wataalamu mnaowahitaji kutengeneza wataalamu wa kuandaa mtaala huo hii ni kuonesha kwamba sisi kama DIT tuko tayari kuwasaidia," alisema Dk Matiko.

Kwa upande wake Kepten Hassan Mwendwa alisema kuwa lengo la kuamua kuandaa mtaala huo ni baada ya wanajeshi wengi wamesomea mambo mbalimbali ikiwemo ya uhandisi umeme lakini tatizo  wanapotoka nje ya Jeshi hawana vyeti vinavyotambulika.

"Kama tunavyojua wataalamu mbalimbali wanaohitajika wapo jeshini lakini tatizo ni kwamba mafunzo yetu ni ya Kijeshi, tunapokua nje ya Jeshi hatuna vyeti vinavyotambulika hivyo tukaona tuanze na hili kwa kutengeneza mitaala ili wataalamu wasome na kuhitimu kama wanavyofanya katika vyuo vingine," alisema Kepten Mwendwa.

Alisema jeshini Wana wataalamu wa kutosha, vifaa vya kutosha  ambavyo vitawasaidia katika mafunzo hayo na kwamba uzuri ni kwamba jeshini wanajifunza zaidi kwa vitendo.

Kwa upande wake Kepteni Faida Sibora alitoa shukran kwa niaba ya Jeshi la Wananchi kwa msaada walioupata kutoka DIT na kuahidi kuendelea kushirikiana.

DIT imejipambanua katika kutoa utaalamu ambao unatatua matatizo katika jamii na kutoa wataalamu wa hali ya juu katika kutimiza azma ya serikali ya kufikia uchumi wa kati kupitia viwanda.
 Kaimu Mkuu wa Chuo Tafiti na Taaluma, Dk Ezekiel Amri akiendesha kikao cha pamoja kati ya maofisa wa Jeshi la Wananchi na Taasisi ya Teknolojia Dar es Salaam (DIT)
Kaimu Mkuu wa taasisi (ignore chuo weka Taasisi) Taaluma na Mafunzo, Dk Ezekiel Amri katika picha ya pamoja na Wakufunzi wa Shule ya Kijeshi ya Ulinzi wa Anga Tanga (SKUA) na wafanyakazi wa DIT.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...