
Ufafanuzi huu unafuatia maoni na malalamiko yaliyotolewa na
wanafunzi wa vyuo mbalimbali, kikiwemo Chuo Kikuu cha Dar es salaam (CKD) kuhusu
malipo ya fedha za vitabu na viandikwa (books and stationery) na malipo ya chakula
na malazi (meals and accommodation) kwa wanafunzi waliobadilisha kozi.
Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya HESLB Prof. William A.L.
Anangisye ametoa ufafanuzi huu leo (Jumatatu, Desemba 16, 2019) jijini Dar es
salaam katika kikao cha pamoja kati yake, menejimenti ya HESLB, menejimenti ya
CKD na wawakilishi wa viongozi wa wanafunzi wa CKD.
“Wanafunzi wote wa taasisi za elimu ya juu wanapokutana na
changamoto wasisite kuziwasilisha kwa menejimenti za vyuo ambavyo
vitaziwasilisha HESLB au kwa taasisi sahihi, hata nyie mlipaswa kuanzia kwetu
na tungeyafanyia yote kazi badala ya kutoa maelekezo ya masaa 72,” amesema
Prof. Anangisye ambaye pia ni Makamu Mkuu wa CKD.
Kikao hicho pia kilihudhuriwa na Mkurugenzi Mtendaji wa HESLB
Abdul-Razaq Badru, Naibu Makamu Wakuu wa CKD, Prof. Killian Bernadetha
(Utafiti), Prof. David Mfinanga (Utawala), wawakilishi wa serikali ya wanafunzi
CKD na watendaji wengine wa CKD na HESLB.
Akizungumza katika kikao hicho, Mkurugenzi Mtendaji wa HESLB
Abdul-Razaq Badru amesema kwa sasa HESLB inakamilisha malipo ya fedha za
wanafunzi waliobadilisha kozi ambayo imepokelewa na HESLB kutoka Tume ya Vyuo
Vikuu (TCU) mwishoni mwa wiki na fedha hizo zitawafikia wanafunzi ifikapo
keshokutwa, Desemba 18 mwaka huu.
“Kuna kundi la wanafunzi waliobadilisha kozi wakiwa vyuoni na
taarifa hizo zilikua hazijatufikia, tumezipokea mwishoni mwa wiki na
tunakamilisha malipo ambayo yatawafikia siku mbili zijazo,” amesema Badru na
kufafanua:
Kwa mujibu wa Badru, kundi jingine linahusu malipo ya vitabu
na viandikwa, ambapo malipo ya awamu ya kwanza ya jumla ya TZS 13.3 bilioni
yameshafanyika na awamu ya pili ya TZS 1.1 bilioni itawafikia wanafunzi ifikapo
jumamosi ijayo, Desemba 21 mwaka huu kwa kuwa wataalamu wetu wanakamilisha
uchambuzi,” amesema.
Kwa upande wao, viongozi wa wanafunzi walioongozwa na Hamis
Mussa walishukuru kwa kupata fursa na kuwasilisha masuala yao na kupata
ufafanuzi.
Hadi sasa, jumla ya
wanafunzi 49,485 wa mwaka wa kwanza wameshapata mikopo yenye thamani ya TZS 169.4
bilioni na kuvuka lengo la kutoa mikopo kwa wanafunzi wa mwaka wa kwanza wapatao
45,000. Kati yao, wanafunzi yatima waliopoteza mzazi au wazazi wote wawili ni 10,383,
wenye ulemavu (397), waliofadhiliwa masomo ya sekondari (3,128) na wengine
wahitaji 35,577. Aidha, wanafunzi 78,337 wanaoendelea na masomo wamepata mikopo
yenye thamani ya TZS 272.1 bilioni.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...