Mkuu wa Kitengo cha polisi jamii mkoa wa Arusha SSP Joswam Kaijanante


Na.Vero Ignatus,Arusha.

Matukio ya unyanyasaji wa Kijinsia mkoani Arusha yameendelea kuongezeka kutoka matukio 2456 ya mwaka 2018 hadi kufikia 4334 mwaka 2019 licha ya elimu mbalimbali kuendelea na wadau kutolewa kukabiliana na matukio hayo.

Mrakibu Mwandamizi wa polisi SSP Joswam Kaijanante ambaye pia ni mkuu wa kitengo cha polisi jamii mkoa wa Arusha alisema jumla ya matukio 4334 yametokea mkoani hapo kwa upande wa kina mama,watoto ,wakiwemo wanaume pia katika kipindi cha mwaka 2019.

Alisema kuwa licha ya matukio hayo kuongezeka makosa yanahusiana na unyanyasaji wa kijinsia ni pamoja na ulawiti na kubaka yamepungua ambapo kubaka ni makosa 161 yaliyoripotiwa januari -septemba 2018,ambapo januari -septemba 2019 yalikuwa makosa 82,tofauti ni 79.

Alisema, makosa ya ulawiti yaliyoripotiwa Januari-septemba mwaka 2018 makosa 61 huku mwaka 2019 yaliripotiwa makosa 52 tofauti ni 9.

Alisema makosa ya kutoa mimba yameongezeka ambapo mwaka 2018 yaliripotiwa makosa 31 ambapo mwaka 2019 yaliripotiwa makosa 49 tofauti ni 18

Makosa ya kumpa mimba mwanafunzi nayo yameongezeka ambapo yaliyoripotiwa kuanzia januari -septemba 2018 yalikuwa jumla ya makosa 169, ambapo januari -septemba 2019 yaliripotiwa makosa 177 tofauti ni makosa 8.

Pia makosa ya Kumtorosha mwanafuzi yameongezeka na kwamba yaliripotiwa mwaka 2018 jumla ya makosa 30 ambapo mwaka 2019 jumla ya makosa 32 yameripotiwa na kufanya ongezeko la makosa 2.

Alisema, pia kuna makosa ya kushindwa kumuhudumia mwanafunzi ambapo mwaka 2018 yaliripotiwa makosa 889 ambapo mwaka 2019 yamepungua na kuwa makosa 32 pungufu ya makosa 857.

utumia lugha ya matusi januari-septemba 2018 jumla ya makosa 178 ambapo januari-septemba 2019 jumla ya makosa 922 tofauti 746

Kutishia kuua januari -septemba 2018 jumla ya makosa 110 yaliripotiwa ambapo januari-septemba 2019 yaliripotiwa jula ya makosa 840 tofauti ni makosa 730,kujaribu kubaka januari -septemba 2018 jumla ya makosa 104 yaliripotiwa ambapio januari -septemba 2019 jumla ya makosa 43 tofauti ni makosa 61.

Kujeruhi januari -septemba 2018 jumla ya makosa 231 ambapo januari -septemba 2019 yaliripotiwa makosa 765 tofauti ni makosa 534.Shambulio januari-septemba 2018 jumla ya makosa 349 yaliripotiwa ambapo januari -septemba 2019 1191 tofauti 842.

Kufanya mapenzi na mwanafunzi januari -septemba 2018 jumla ya makosa 1 ambapo januari -septemba 2019 jumla ya makosa 0 tofauti yake ni 12

Kumtorosha mwanafunzi januari -septemba 2018 jumla ya makosa 34 yaliripotiwa ambapo januari -septemba 2019 yaliripotiwa jumla ya makosa 10 tofauti 24,kujaribu kujiua januari -septemba 2018 jumla ya makosa 45 yaliripotiwa ambapo januari -septemba 2019 jumla ya makosa 16 tofauti ni makosa 29.

Wizi wa watoto januari-septemba 2018 jumla ya makosa 5 yaliripotiwa ambapo Januari -septemba 2019 jumla ya makosa 3 tofauti ni 2.

Kutelekeza familia januari -septemba 2018 jumla ya makosa 51 ambapo januari -septemba 2019 jumla ya makosa 102 tofauti ni makosa 51.

Kujinyonga januari -septemba 2018 juimla ya makosa 5 yaliripotiwa ambapo januari -septemba 2019 jumla ya makosa 13 yaliripotiwa tofauti ni makosa 8,Kukeketa januari -septemba 2018 jumla ya makosa 2 yaliripotiwa ambapo januari -septemba 2019 jumla ya makosa 0 tofauti ni 2.

Kutupa watoto januari -septemba 2018 jumla ya makosa 1 liiripotiwa ambapo januari -septemba 2019 jumla ya makosa 5 tofauti ni makosa 5,ambapo inaleta idadi ya makosa 2456 kwa mwaka 2018 ambapo mwaka 2019 jumla ya makosa 4334 tofauti 1878.

SSP Joswam Kaijanante alisema kuwa pia wanataarifa ya baadhi ya wazazi ambao wamebuni mbinu ya kuwakeketa watoto wachanga ambapo bado wanaendelea na uchunguzi atakayebainika sheria itachukua mkondo wake

Amesema wanaendelea kuielimisha jamii kwani jambo hilo la kukeketa watoto linafanyika kwa usiri mkubwa mtoto akiwa bado mchanga ni vigumu sana kubaini suala hilo

Amesema dawati ngazi ya mkoa linashirikiana na Ustawi wa jamii kwenye Halmashauri kwasababu wao wana watu hadi kwenye ngazi ya kata sambamba na mashirika yasiyo ya Kiserikali ambayo yanashughukika na kupinga ukatili dhidi ya vitendo vya unyanyasaji haswa wakina mama na watoto.

Amesema changamoto kubwa iliyopo kwenye unyanyasaji watu wengi wanaofikiria kwa mwanamke na mtoto tu ila wanaume

"Wanaume wananyanyaswa ila wanakuwa waoga kusema wanaona aibu kwamba jamii inayowazunguka itawachukuliaje"alisema Kaijanante

Alisema kuwa wanaendelea kuielimisha jamii ili kama wanaume wananyanyaswa watoe taarifa ,wanaume wengi wanaumia sana na wananyanyaswa,ila kwa sasa mwamko mkubwa upo kwani baadhi ya wanaume wanaripoti matukio ya kunyanyaswa ila tunawahakikishia kuwa tunayashughukikia kwa kiasi kikubwa sana.


Aidha wanaume wameaswa kujitokeza kutoa taarifa pale wanapofanyiwa unyanyasaji wa kijinsia kwani dawati hilo ngazi ya mkoa wanafanya mazungumzo kwa njia ya usiri mkubwa ambao utawafanya wanaume hao kuwa salama

Kwa upande wake Insp.Lucia Mpakaseke alitaja baadhi ya unyanyasaji wa Kisaikolojia kuwa ni pamoja na matendo yanayosababisha maumivu ya kihisia ,kiakili,au kutishia kufanya fujo ,maneno ya fedheha,dharau na kutishia kutoa siri hadharani.

Alisema kuwa zipo baadhi ya ndoa nyingine ambazo kuna siri wanazifahamu wenyewe ,ila inapofikia mahali wakatofautiana mmoja wapo anatishia kuitoa siri hiyo hadharani ambapo kisaikolojia/kiakili humuathiri mmojawapo.

Matendo mengine ni pamoja na kunyang'anywa watoto,kutishiwa kuuwawa pale ambapo linatokea tatizo badala ya kusuluhisha wanatishiana,wivu wa kupindukia,ukatili wa kingono,ndoa za utotoni,usafirishaji wa mabinti kwaajili biashara za ngono,kulazimishwa kufanya biashara za ukahaba.

Aidha amesema Ukatili mwingine ni wa mila na desturi mfano ukeketaji,kuchumbia watoto wakiwa wadogo kwa baadhi ya makabila kwa kuchukua mahari,mauaji ya vikongwe,walemavu wa ngozi,matambiko ya kingono kwa watoto.

Ukatili wa kiuchumi ambao unamnyima fursa za kimaendeleo mtoto wa kike kushiriki katika maendeleo,kukatazwa kufanya kazi,unyanyasaji wawasichana au wasaidizi wa kazi majumbani,walemavu,waathirika wa VVU na Ukimwi.

Tanzania imeungana na nchi nyingine duniani katika maadhimisho ya siku 16 ya kupinga Ukatili wa kijinsia ambapo yalizinduliwa rasmi mkoani Dodoma ma Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia na watoto nchini Ummy Mwalimu ambapo kilele chake kitakuwa Desemba 10,2019 ambapo Kauli mbiu katika maadhimisho hayo ni Kizazi chenye Usawa:Simama dhidi ya Ubakaji.


Ambapo lengo kuu la maadhimisho hayo ni kuongeza ushawishi kubadilishana taarifa,uzowefu wa kujenga uwezo wa pamoja,kuelimisha,kukemea,kuchukua hatua kwa pamoja ili kupinga ukatili wa kijinsia.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...