Wafanyabiashara na wajasiriamali wametakiwa kulinda/kuwa na nembo za bidhaa ili kuweza kuingia kwenye soko la ushindani  pasipokuwa na changamoto zisizo za lazima.

Akizungumza katika kongamano la kiuchumi la wanawake wa Mkoa wa Arusha lililofanyika jijini Arusha Msaidizi wa Usajili Mkuu Wakala ya Usajili wa Biashara na Leseni (BRELA) Lumambo Shiwala amesema kuwa wafanyabiashara na ambao wanataka kupata fursa anawahimiza kusajili ili  kulinda alamazao za biashara maana asije akapoteza juhudi zake zote katika kuandaa biashara yake.

"Hata kama unatengeneza sabuni ama kitu chochote hakikisha utambulisho au nembo umeilinda kisheria na taasisi inayoshughulikia na kulinda kisheria biashara au nembo ni BRELA". Amesema Bw.Shiwala.

Aidha Bw.Shiwala amesema kuwa mahitaji ya kusajili jina la biashara kwa sasa hivi ni kitambulisho chako cha taifa peke yake.

"Mfanyabiashara au mjasiriamali ambaye atatakiwa kuingia kwenye ushindani atatakiwa kuwa na jina lake pekee ili kusudi kulitambulisha kwa wateja wake kwahiyo msiingie kwenye biashara bila kulisajili jina lako maana anaweza kulichukua mtu mwingine na kulisajili na kuwa mali yake". Amesema Shiwala.
Msaidizi wa Usajili Mkuu Wakala ya Usajili wa Biashara na Leseni (BRELA) Lumambo Shiwala akizungumza katika kongamano la kiuchumi la wanawake wa Mkoa wa Arusha lililofanyika jijini Arusha.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...