Makundi
yaliopo ndani ya chama cha mapinduzi mkoa wa Arusha yanasababishwa na
baadhi ya viongozi ambao sio waadilifu katika chama hicho mkoani Arusha
Hayo yameelezwa na katibu wa Itikadi na Uenezi taifa Wa chama cha mapinduzi Hamphrey Polepole
ambaye pia ni mlezi wa CCM Mkoa wa Arusha wakati akiongea na wajumbe
Wala chama cha mapinduzi mkoa Wa Arusha wakati katika mkutano maalumu Wa
uchaguzi Wa Mwenyekiti Wa CCM mkoa ambapo alisema kuwa makundi yaliopo
ndani ya chama hicho yanasababishwa na baadhi ya viongozi Wa serikali na
chama wasio waadilifu
Alisema
wanachama Wa chama hicho hawana makundi wala magenge ,ila baadhi ya
viongozi ambao sio waadilifu,wasiotaka kutekeleza ilani ya chama cha
mapinduzi, wanaoweka maslayi yao mbele badala ya maslayi ya chama ndio
wanaunda makundi na kutengeneza magenge ya kuboma chama badala ya
kujenga.
"Niwaombe wana
Arusha tuache makundi tukijenge chama chetu,tusikubali baadhi ya
viongozi wasiokitakia chama chetu mema wakawatengenezea makundi ndani ya
chama nataka kuona Arusha yetu ikiwa tulivu ,ikiendelea kuwa ya
kijani,majimbo yote yakiongozwa na CCM ,na serikali ikiendelea
kuendeshwa na chama chetu na hii italetwa na umoja wetu,na sio makundi
ya wanachama au viongozi" alisema Polepole
Alibainisha
kuwa yeye kama mlezi Wa chama hicho mkoa Wa Arusha hatamfumbia macho
kiongozi yeyote au mwanachama ambaye ataendekeza ,au ataongoza kuunda
makundi katika chama hicho ,kwani wanataka makundi yaishe ili chama
hicho kiweze kuendelea kuongoza serikali na kuwaletea wananchi
maendeleo.
Kwa upande wake Mwenyekiti Wa CCM mkoa Wa Arusha Zelothe Steven Zelothe alitoa
massa 48 kwa viongozi pamoja na wanachama Wa chama hicho wale wenye
makundi kuyavunja Mara moja kwani wasipofanya hivyo na wakabainika hatua
Kali zitachukuliwa dhidi yao.
Alisema
kuwa Kazi kubwa ambayo anaifanya nikukijenga chama cha mapinduzi mkoa
Wa Arusha ,kuyafuta Makundi na makambi yote ambayo yapo ndani ya chama
hicho ,kwani kwakufanya ivyo atajenga chama imara chenye wanachama imara
watakayo weza kuilinda na kuiongoza nchi.
"Makundi
na makambi yanaleta msuguano kwenye maofisi,kusengenyana had I
kupelekea kazi kitofanyika vizuri lakini Mimi sitakubali jambo hilo
litokee kwakweli "Zelothe
Alibainisha
amejipanga kushirikiana na idara zote za serikali,taasisi binafsi
,viongozi Wa dini ,wananchi wote bila kuchagua hali yake kiuchumi ,huku
akisisitiza kuwa atawapa ushirikiano zaidi wanyonge kwa kutatua kero
zao,atasimamia na kutatua kero za wananchi na hii itasaidia kuendelea
kujenga chama hicho.
Naye
kada Wa Ccm aliejitambulisha kwa jina LA Tausi Swalehe alisema ni
kweli wanachama Wachama hicho hawana makundi ila kunabaadhi ya viongozi
ambao sio waadilifu ndio wanatengeneza makundi ndani ya chama hicho.
Alibainisha
kuwa nivyema wakaacha Mara moja tabia hiyo na kuanza kuwa pamoja na
kujenga chama kimoja kitakacho waletea wananchi maendele
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...