Baadhi ya wafungwa wakiume wa Gereza Kuu Butimba walionufaika na Msamaha
wa Rais wakitoka katika lango la Gereza Kuu Butimba tayari kwenda
kuungana na familia zao. Wafungwa hao wamemshukru Rais Magufuli kwa
msamaha huo wa kihistoria.
Kamishna Jenerali wa Magereza nchini, CGP - Phaustine Kasike akitoa
taarifa fupi ya zoezi zima la uachiliaji wa wafungwa walionufaika na
msamaha wa Rais katika mikoa mbalimbali nchini mbele ya wanahabari
kutoka vyombo mbalimbali vya Habari jijini Mwanza leo Desemba 10, 2019.
Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Mhe. John Mongela ambaye pia ni Mwenyekiti wa
Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa huo akizungumza na Wafungwa wa
Gereza Kuu Butimba kabla ya zoezi la uachiliaji wa wafungwa walionufaika
na Msamaha wa Rais leo Desemba 10, 2019. Kushoto ni Kamishna Jenerali
wa Magereza nchini, CGP - Phaustine Kasike.
Kamati ya Ulinzi na Usalama Mkoani Mwanza pamoja na Kamishna Jenerali
wa Magereza nchini, Phaustine Kasike wakishuhudia wafungwa walionufaika
na Msamaha wa Rais katika Gereza Kuu Butimba wakipewa mali zao na nauli
ya kwenda kuungana na familia zao leo Desemba 10, 2019 kabla ya zoezi la
uachiliaji wa wafungwa husika wa msamaha huo.
Kamishna Jenerali wa Magereza nchini, CGP - Phaustine Kasike(wa pili
toka kulia) akiteta na Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Mhe. John Mongela(vazi la
kitenge) ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi na Usalama ya
Mkoa wa mwanza alipowasili gereza Butimba kushuhudia zoezi la uachiliaji
wafungwa walionufaika na msamaha wa Rais.
Mfungwa mnufaika wa Msamaha wa Rais, William Dingu akizungumza na Wanahabari(hawapo pichani) baada ya kuachiliwa huru leo. Mfungwa huyo amemshukru Rais kwa msamha huo, aidha, amelipongeza Jeshi la Magereza kwa kumwezesha ujuzi wa wa fani ya ujenzi ambao ameupatia gerezani kupitia programu ya Urekebishaji inayosimamiwa na Jeshi hilo(Picha zote na Jeshi la Magereza).
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...