Na, Editha Edward -Tabora
Wananchi
mkoani Tabora wametakiwa Kujiunga na mfuko wa afya ya jamii
Iliyoboreshwa (CHF) jambo ambapo litawasaidia kupata huduma ya afya kwa
bei nafuu ya shilingi elfu thelathini kwa kila Maya watu sita
Ameyaeleza
hayo mkuu wa mkoa huo Aggrey Mwanri wakati akizungumza na waandishi wa
habari ofisini kwake na kuwasisitiza wananchi Kujiunga na mfuko huo wa
afya na kuwahakikishia upatikanaji wa dawa
Mwanri
amesema mfuko huo utawasaidia wananchi wenye kipato cha chini kuweza
kupata huduma ya afya kila mahali hapa nchini ukitofautisha na zamani
ambapo mwananchi alipokuwa akijiunga kwa ajili ya kupata huduma ya afya
ndipo anapotibiwa
"Mtu
yeyote unapojiunga na mfuko huwa afya ya jamii Iliyoboreshwa utatibiwa
nchi nzima uwe bodaboda mama ntiliye mjasiriamali mkulima na kila Mtu
atapata dawa kulingana na maelezo ya daktari "Amesema Mwanri
Aidha
Mwanri ametoa onyo kwa watumishi ya sekta ya afya ambao watahusika kwa
kukwamisha zoezi hili kwa kuwabugua watu walio jiandikisha hatua kali
zitachukuliwa hasa kwa upande wa Rushwa kwani ni kinyume na maadili
Kwa
upande wake Afisa ustawi wa jamii ofisi ya mkuu wa mkoa wa Tabora
Baraka Mackona amebainisha jinsi ya Kujiunga na mfuko huo kwa wananchi
ni kufika katika serikali za mitaa na kujiandikisha ili kupata huduma
hiyo
Aidha jumla ya Kaya
elfu sita zimeshajiunga na mfuko wa (CHF) Iliyoboreshwa kwa mkoa mzima
wa Tabora na zinaendelea kufaidika na huduma zinazotolewa na mfuko
huo.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...