*Yasaidia wananchi wasiojiweza milioni 41 kwa ajili ya kugharamia matibabu

Na Chalila Kibuda Globu ya Jamii,Arusha
HOSPITALI ya Rufaa ya Mkoa wa Arusha Mount Meru imesema  kwa mwezi mmoja pekee inatumia Sh.milioni 41 kuwahudumia takribani wagonjwa  3,224 wasio na uwezo wa kuchangia matibabu.

Pia imesema kila mwezi inatoa matibabu kwa njia ya upasuaji kwa wanawake 200 wanaojifungua hiyo ikiwa ni wastani wa asilimia 34  ya wanawake wanaojifungua kwa njia ya upasuaji.

Hayo ameyasema  Mganga Mfawithi wa Hospitali hiyo Dkt.Shafii Msechu wakati akizungumza  mafanikio ya Mount Meru chini ya utawala wa Rais Dk John Magufuli  ikiwa ni utekelezaji wa Kampeni ya Tumeboresha sekta ya afya.

Kampeni hiyo inalenga kuonyesha mafanikio na mikakati iliyopo katika taasisi zote zilizo chini ya wizara ya Afya Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto.

Dkt.Msechu amesema hospitali hiyo inahudumia  makundi yote ya wagonjwa akitaja watu wenye uwezo wa kuchangia huduma na wasio na uwezo.

Akizungumzia  idadi ya wanawake wanaojifungua katika Hospitali hiyo Dkt.Msechu amesema "Idadi hii ni kubwa kutokana na hospitali kuwa ya rufaa na idadi kubwa ya wagonjwa wanaoshindikana kupatiwa matibabu  hospitali ngazi za chini wanaletwa Mount Meru  "amesema.

Kwa upande wa huduma za dharura Dk.Msechu amesema  mpaka sasa zaidi ya wagonjwa 38,000 wamepatiwa huduma.

"Kwa kushirikiana na mdau wa maendeleo tumefanikiwa kujenga kitengo cha dharura na imesaidia kupunguza vifo 12 mpaka kufikia 7  na hii ni kutokana na uwepo wa huduma ya dharura " amesema.

Pia Dk.Msechu amesema hali ya upatikanaji wa dawa katika hospitali hiyo ni asilimia 85,huku wakiwa wanatumia asilimia 65 ya mapato yao ya ndani kwaajili ya kuongeza dawa zitakazohitajika.

"Tumetenga fedha nyingi kwaajili ya kununulia dawa asilimia 59 ya fedha za bima tunazielekeza kwenye dawa ,asilimia nyinginezo tunaongezea, sisi dawa tunanunua kupitia Bohari Kuu ya Dawa (MSD) dawa  ambazo hawana tunanunua kwa mshitiri"alisema 

Kwa upande wa mapato Dkt.Msechu amesema  mfumo upatikanaji  wa dawa   umewasaidia kuongeza mapato.

"Miaka ya nyuma tulikuwa tunapata sh milioni 80 mpaka 120 lakini sasa tunapata sh milioni 331 na mfumo ndio umesaidia tukafika hapa"alisema.

Katika hatua nyingine Dk.Msechu amesema mount meru ina mpango wa kuanzisha matibabu ya figo na tayari wana mashine tano kwaajili ya zoezi hilo na hatua waliyonayo sasa ni ujenzi wa jengo la kutolea huduma hiyo .

Akizungumzia huduma za dharura 
Afisa muuguzi wa hospitali hiyo Simphorosa Silalye amesema kuwepo kwa kitengo hicho kumesaidia kwa kiwango kikubwa kupunguza vifo kwa wagonjwa waliokuwa wakifikishwa  hospitalini hapo ambapo kundi kubwa linatokana na ajali.

Saitoti Salomon mkazi wa Sekei amesema huduma za afya chini ya Rais Dk.John Magufuli zimeboreshwa kwa kiwango kikubwa.

"Tunachoomba ni yale magonjwa ambayo hajaorodheshwa kwenye bima waweke ili kuturahisishia au kutuletea unafuu kwa sasa ukiwa na bima alafu magonjwa mengine hutibiwi haisaidii"alisema .
 Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa ya Mount Meru Dkt.Shafii Msechu akizungumza na waandishi wa Habari kuhusiana namna walivyoboresha huduma za afya kutokana  na serikali kuwekeza katika Hospitali hiyo. 
Mkuu wa Msafara na Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini wa Wizara ya Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Gelard Chami akizungumza kuhusiana Kampeni ya  Tumeboresha sekta ya Afya ambayo lengo ni kuangalia mafanikio ya sekta hiyo.
 Dobi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa Mount Meru Samwel Abraham akizungumza kuhusiana mashine mpya ya kufulia ambazo Serikali imeziweka katika Hospitali hiyo.
 Afisa Muuguzi wa Magonjwa ya Dharula wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa Mount Meru Simphorosa Silalye akitoa maelezo kuhusiana wanavyokoa maisha katika hicho tofauti na miaka ya nyuma.
 Wananchi wakiungia na kutoka katika Hospitali Rufaa ya Mkoa Mount Meru,Arusha
 Mtaalam wa Miozi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa Mount Meru Lutenta Melkzedec akionesha mashine ya kisasa Miozi I iliyofungwa Hospitali ya Mount Meru.
Afisa Muuguzi Mfawidhi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa  Mount Meru ,Arusha Beatrice Mndeme akitoa maelezo kuhusiana na mafanikio ya mashine za ufuaji.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...