Pichani Maalim Seif alipokuwa akichukua kadi namba moja ya chama cha ACT-Wazalendo kipindi alipojiunga na chama cha ACT-Wazalendo rasmi.
Picha kwa hisani ya Mtandao.

Na Mwandishi wetu, Globu ya Jamii
Aliyekuwa Katibu Mkuu wa Chama cha Wananchi (CUF), Maalim Seif Sharif Hamad, leo kuchukua fomu ya kugombea uongozi kitaifa ndani ya chama cha ACT- Wazalendo.


 Hii ni baada ya Chama hicho kukamilisha chaguzi katika ngazi za chini.

Maalim Seif  atachukua fomu leo na kurejesha fomu kwa kuwania nafasi ya   uongozi katika ngazi ya Taifa  ambapo tangu Januari, 27 hadi 26 Februari, 2020 fumu zilianza kuchukuliwa na wanaowania nafasi mbalimbali za uongozi.

Hivyo leo saa tano huko Vuga, Zanzibar Maalim Seif Sharif Hamad atachukuafomu ya kugombea nafasi mojawapo kati ya nafasi za uongozi zilizotangazwa kugombewa katika Chama Cha ACT Wazalendo

Kwa taarifa hii, ndugu waandishi wa habari mnaalikwa rasmi kushuhudia Baada ya kuchukua fomu hiyo, Maalim Seif  atazungumza na waandishi wa habari kuhusu dira na mwelekeo wake juu ya nafasi ya uongozi anayokusudia kuiomba katika Chama cha ACT-Wazalendo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...