Na Ahmed Mahmoud Arusha .

Mamlaka ya mawasiliano nchini TCRA Kanda ya kaskazini imewataka mafundi wa vifaa vya kieletroniki ikiwemo simu za mkononi kuwa kwenye mfumo wa umoja kwa kuanzisha vikundi vyao kwa Kanda au mkoa.
Kwa muktadha huo kuanzia mwezi julai mwaka huu hakuna fundu ambaye atafanyakazi kama hajasomo wala kusajiliwa hivyo ni muhimu kwenu kujiunga kwenye kikundi ili kupatiwa elimu. 

Kauli hiyo imetolewa na Mwanasheria wa mamlaka hiyo Kant Mosha wakati wa mkutano wa mafundi wa vifaa vya kieletroniki uliofanyika kwenye ukumbi wa ofisi ya mkuu wa mkoa wa Arusha ambapo aliwataka kuacha kutokuwa na usajili wa kikundi ndio suluhisho. 

Alisema kuwa mafundi simu ni kada ambayo ilikuwa imesahauliwa hapo awali lakini kupitia serikali ya awamu ya tano chini ya Rais dkt.John Magufuli imeamua kuwatambua hivyo kuungana ni sehemu ya kufanikiwa kwa malengo yenu. 

Kwa upande wake Mwenyekiti wa chama cha mafundi simu Kanda ya ziwa Maguwa Manyanda amewataka kutambua kwamba mafundi simu ni wathamani kwani jamii inwategemea na wanachangia mapato ya serikali hivyo busara ni kuona umoja ndio suluhisho la changamoto zao.
Alisema kuwa mafunzo hayo yataondoa changamoto na kuwafanya kuwa huru katika shughuli zao za kila siku hivyo umoja ni nguzo ya kuwafikisha kuweza kushirikiana na serikali katika masuala mbalimbali ikiwemo vyombo vya Dola. 

Alieleza kuwa kufanikiwa ili kila moja aweze kutenda kazi zake ni muhimu Sana wakajiunga na umoja ili kuondoa changamoto zao ambazo zimekuwa zikiwafanya kujikuta wakikumbana na jeshi la polisi.
Nae Mwenyekiti wa umoja wa mafundi simu Kanda ya kaskazini Nasri Mshana Mtengeti alisema kuwa wamefirahi Sana kupata elimu hiyo ya umoja ambayo itawasaidia kuondokana na changamoto hivyo tuhamasishane kujiunga na umoja huu. 

Awali akitoa mafunzo kwenye mkutano huo mratibu wa vikundi hivyo kutoka mamlaka ya mawasiliano mhandisi Kadaya Buluhye aliwataka mafundi hao kufanyakazi kwenye umoja kwa lengo la kupata elimu na usajili. 

Alisema kuwa jeshi la polisi linafanyakazi ya kulinda usalama na Mali za raia Ila umoja wenu utasaidia kufanya kazi kwa karibu na jeshi hilo na kuondoa changamoto zenu ambazo mmekuwa mkikumbana nazo kama mafundi.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...