Rawan Dakik akizungumza na wanahabari nje ya jengo la TANAPA.
 Mama mzazi wa Rawan, Hala akiongea na waandishi wa habari.

Na Woinde Shizza, Arusha
MFAHAMU msichana mdogo wa kitanzania aliezaliwa mkoani Arusha alieweza kupanda milima sita mirefu duniani na mwezi march anaenda kutimiza ndoto zake kwa kupanda mlima mkubwa kuliko yote Mlima Everest ni mlima mkubwa kabisa duniani, wenye kimo cha m 8,848 juu ya usawa wa bahari, Ni sehemu ya safu ya milima ya Himalaya Kilele chake kipo katika mpaka wa Nepal na China (Tibet).

Msichana Rawan Dakik ni msichana wa kitanzania mwenye umri wa miaka 18 msichana huyu ni mtoto wa tatu kutoka kwa mama yake aliyejulikana kwa jina la Hala Dakik ,msichana huyu alianza kupanda mlima ndani ya nchin ya Tanzania akiwa anaumri wa miaka 12 baada ya kujiunga na timu ya shule ya upandaji milima ambapo alipata elimu ,ujuzi na taarifa mbalimbali za milima duniani.

Baada ya kupata mafunzo haya msichana huyu alivutiwa sana na mchezo ya kupanda na kujua kuhusu milima hivyo akaamu kuweka rekodi ya kupanda milima yote saba mirefu kutoka katika mabara saba duniani na aliaanza akiwa na umri mdogo sana.

Msichana Rawan  akizungumza na mwandishi wa MICHUZI BLOG  kuwa ni uamuzi wake mwenyewe uliomfanya kuanza michezo hiii yakupanda milima na uhamuzi wake huu ulizingatia kutoharibu masomo yake na ufaulu wake katika masomo.

Amebainisha kuwa ndoto yake imekuwa kweli mpaka sasa ameweza kupanda milima sita katika mabara manne na kupeperusha bendera katika kila kilelel, aliweza kupandisha bendera mbili moja ikiwa ya nchi yake ya Tanzania huku bandera ya pili ikiwqa Amani ya dunia .

Amesema kuwa lengo lake haswa ni kufikisha ujumbe wa kutaka amani duniani, kuhamasisha maendeleo kwa wanawake na vijana wa rika lake na kuwataka wajitahidi kutimiza ndoto zao na kufahamu kuwa ukiwa na nia chochote kinawezekana.

Ametaja baadhi ya milima aliyoipanda kuwa ni pamoja na Kilimanjaro uliopo hapa Nchini Tanzania katika bara la Afrika na una urefu wa mita 5,895 mlima mungine ni Elbras uliopo nchini Urusi barani Ulaya wenye urefu wa mita 5,648, mwingine ni Aconcagua uliopo nchni Argentina barani Amerika ya kusini wenye urefu wamita 6,961 pamoja na Carstenz Pyramid uliopo nchini Indonesia ndani ya bara la Asia wenye urefu wa
mita 4884, pia amepanda mlima uliomrefu zaidi katika bara la Antartica karibu kabisa na nchin ya Chile wenye urefu wa mita 4,892.

Ili aweze kupanda milima hii ametakiwa kufanya mazoezi masaa ishirini kwa wiki na mazoezi haya yatampa uwezo wa kubeba mzigo wake mwenyewe wenye kilo thelathini na tano (35 kg) na kuvuta mwingine wenye vifaa vya kupandia mlima wenye uzito wa kilo 30 kufanya mazoezi ya
kuhimili kupanda mlima katika hali ya hewa ya chini ua kiwango cha baridi cha nyuzi 30c ,na hivi sasa anaendelea na mazoezi hayo ambapo amesema mwezi machi mwaka huu anampango wa kupanda mlima mrefu kuliko yote duniani ujuliokanao kwa jina la Everest”.

Ametaja milima mingine ambayo ameipanda ni pamoja na mlima wenye baridi kali wa Kazbek wenye urefu wa mita 5,o33  ulioko Georgia nchini Urusi kama sehemu ya mazoezi, Aidha ameweza kupanda katika vilelel vya milima miwili iliyopo mkoani Arusha Tanzania na kilele cha
mlima mmoja uliopo nchini Uganda hii yote ni sehemu ya mazoezi ya kupanda mlima Everest.

Rawan (17) kufikia kiwango cha kupanda mlima Vinson Massifna mlima Dinal atakuwa amaevunja rekodi mara baada ya kupanda mlima Everest na ataliwa mwanamke wa kwanza kupanda mlima huo akiwa mdogo, pia ndio mtanzania wa kwanza kupanda mlima huo na kuvunja rekodi ya kupanda
milima yote mirefu iliopo katika mabara saba.

"Nafanya mazoezi ya ndani kwa masaa 20 kwa wiki mazoezi yanayonipa uwezo a kubeba mzigo ene kilio hadi kumi na tano kuvuta mwingine wenye uzioto wa hadi kilo 25 ,mazoezi mengine nayoyafanya ni kupanda mlima katika hali ya baridi inayoweza kufikia chini ya kiango cha nyuzi 50, mazoezi haya yamenilazimu kupanda mlima kilimanjaro uliopo Tanzania wenye mita 5,895, mlima wenye baridi kali wa Kazbek wenye urefu wa mita 5,033 uliopo Georgia nchini Urusi ,mlima Rwanzari wenye mita 5,109 uliopo uganda , Mlima Meru wenye mita 4,562 uliopo Arusha Tanzania pmoja na milima midogo eye mita 3,820 katika kuendelea na mazoezi milima mingine niliopanda ni mlima Ararat wene mita 5,137 uliopo Turkey, Mlima kenya enye mita 4,985 uliopo kenya, mlima Qurnat al sada enye mita 3,088 uliopo Lebanon milima yote hii nimepanda ni kwaajili ya mazoezi yakupanda mlima mrefu kuliko yote duniani "amesema Rawan

Rawan amesema kuwa Mlima Everest ni mlima mkubwa kabisa duniani, wenye kimo cha m 8,848 juu ya usawa wa bahari. Ni sehemu ya safu ya milima ya Himalaya Kilele chake kipo katika mpaka wa Nepal na China (Tibet) historia inaonyesha kuwa Watu wa kwanza wa kufika kwenye kilele
walikuwa Edmund Hillary wa New Zealand na sherpa Tenzing Norgay wa
Nepal tarehe 29 Mei 1953 hivyo na yeye anaamini kabisa atafika
kileleni kama hao wa awali walivyofika na kuandika historia ya kwake
na ya nchi yetu kwa ujumla kwani atawekwa kwenye historia za mtanzania
wa kwanza mwanamke na mwanamke wa kwanza kutoka Afrika kuweza
kupanda mlima huo hadi kileleni amebainisha kuwa ataanza safari yake
mwezi ya kupanda mlima mwezi machi mwaka huu na atatumia muda ya
miezi miwili kupanda mlima huo.

Ombi kwa Watanzania
Amesema safari hiyo ni ngumu ila anaamini ataimaliza vyema huku
akiwaomba watanzania wote bila kujali madhehebu yao kumuombea safari
yake ikamilike na aweze kutimiza ndoto zake za kupanda milima yote
mirefu iliopo katika mabara saba duniani, ambapo hadi sasa ameshapanda
milima sita na anaenda kumalizia mmoja.

MAMA WA RAWAN ALONGA
Hala ni mama mzazi wa Rawan amesema kuwa baada ya kugundua ndoto ya
mtoto wao waliamua kumuunga mkono kwa kumpa ushirikiano wa kila hatua ambayo alikuwa akiifanya ili tu mtoto wake atimize ndoto yake.

Amebainisha kuwa wazazi wengi wamekuwa hawataki kufata ndogo za watoto wao waliojiwekea badala yake wamekuwa wakifata vitu ambavyo wao ndio wanavipenda kitu ambacho kinawarudisha nyuma watoto wengi kwani baadhi yao unakuta ana ndoto zake na hafurahi kupangiwa na mzazi wake kitu cha kufanya.

Amesema kuwa mtoto wake alikuwa na malengo (ndoto) za kupanda milima
yote mikubwa duniani na hadi kufikia sasa ameshapanda milima mitano
mikubwa na aliaanza kupanda milima hiyo akiwa na umri wa miaka 12 na
sasa hivi anajiandaa kwenda kupanda mlima mrefu kuliko yote duniani
akiwa kama mtanzania wa kwanza kupanda mlima huo na mwanamke mdogo kuliko wote aliyewahi kupanda mlima huo .

“Tuliona mtoto wetu anandoto na tukaamua kumsapoti na ndio maana hadi
sasa amepanda milima mitano mikubwa Afrika lengo lake ni kupanda
milima yote mikubwa Afrika na sisi lazima tuakikishe amefanikisha
ndoto zake wazazi wenzangu napenda kuwaambia mtoto akiwa na ndoto yake tusiipuuze bali tumsaidie kufikia anapotaka “amesema Hala


Kamishna wa Hifadhi za Tanapa Dk Allan Kijazi anena
Kwa upande wake Kamishna wa Hifadhi za Tanapa Dk Allan Kijazi (TANAPA) Allan Kijazi amempongeza msichana huyo kwa kuweza kupanda milima hiyo ikiwemo Kilimanjaro akiwa na umri mdogo na kumuandi kuwa wao kama TANAPA watampa ushirikiano wa kutosha katika swala zima la
kutimiza ndoto yake.

Amebainisha kuwa pindi msichana huyo akirudi kutoka katika safari yake
ya kupanda mlima huo atakuwa balozi mzuri wa kuutangaza mlima
Kilimanjaro kwa watu mbalimbali, huku akibainisha kuwa msichana huyo
akirudi wataanzisha program ambayo ataifanya kwa kupita mashuleni
kuwahamasisha vijana wenzake kupanda mlima Kilimanjaro.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...