Kikosi cha Simba
Na Yassir Simba, Globu ya Jamii
KLUBU ya Wekundu wa Msimbazi Simba imeendelea kujikita kileleni mwa msimamo wa ligi kuu Tanzania Bara (VPL) mara baada ya hapo jana kuibamiza klabu ya Namungo FC kutoka Ruangwa mkoani Lindi kwa mabao 3 kwa 2
Wekundu hao wa msimbazi Simba wameendelea kujikita kileleni mwa msimamo wa ligi mara baada ya hapo jana kufikisha alama 44 katika michezo 17 waliocheza katika ligi kuu Tanzania bara ( VPL) huku wageni wa mchezo huo timu ya Namungo ikisalia nafasi ya 5 wakiwa na alama 28 mara baada ya kucheza michezo 16.
Mchezo huo ulioanza majira ya saa 7:00 kamili jioni katika uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam huku ikiwachukua dakika 12 Simba Sports Club kupata bao la utangulizi kupitia Kiungo wake mshambuliaji kutoka Kenya Francis Kahata na mnamo dakika 36 ya mchezo mshambuliaji wa Namungo Fc raia wa Burundi Bigirimana Blaise akaisawazishia klabu yake, tukusalia katika kipindi hicho cha kwanza cha mchezo huo Hassan Dilunga akaipatia Simba bao la 2 kwa shuti kali nje ya 18 lilomshinda mlinda mlango wa klabu ya Namungo Nurdin Balora hadi mapumziko Simba 2 Namungo 1
Kipindi cha pili kulianza kwa kasi kwa timu zote mbili kushambuliana ambapo dakika 72 ya mpambano huo Lucas Kikoti kwa shuti kali nje ya 18 alifyatua kombora lilomshinda mlinda mlango wa Simba Beno Kakolanya , Dakia 89 za lala salama za mchezo safu ya ulinzi ya Namungo ikiongozwa na Miza Kristom na Jukumu Kibanda wakidhania Meddy Kagere mshambuliaji hatari wa Simba alikuwa katika eneo la kuotea akawaadhibu bao la 3, mpaka dakika 90 za mchezo huo Simba Sports Club 3 Namungo Football Club 2.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...