Na Bakari Madjeshi, Michuzi TV

Klabu ya Soka ya Azam imesusia mchezo wa Ligi Kuu Soka Tanzania Bara kwa dakika kadhaa baada ya Tanzania Prisons ya Mbeya kusawazisha bao dakika za lala salama (90+4) za mchezo huo uliopigwa kwenye dimba la Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam.

Baada yakuonyesha kususia kuendelea na mchezo huo kwa dakika chache, wakidai na kulalama kuwa bao hilo lililofungwa na Kiungo Mkabaji wa Prisons, Jumanne Elfadhil lilikuwa sio bao halali, Azam FC walirejea tena kwenye mchezo huo.

Katika mchezo huo uliokuwa wa kasi muda wote, timu zote zilikamia kutafuta alama tatu kwa Azam FC kuanza kupata bao lake lakuongoza katika dakika ya 45 kipindi cha kwanza cha mchezo.

Azam FC baada ya sare hiyo, inakuwa sare ya tatu mfululizo baada ya kupata sare ya bao 1-1 na Mtibwa Sugar jijini Dar es Salaam, mchezo wa pili dhidi ya Mbeya City bao 1-1 mjini Iringa katika dimba la Sokoine na ya mwisho dhid ya Prisons katika dimba la Uwanja wa Uhuru.

Baada ya mchezo, Nahodha wa Tanzania Prisons, Benjamin Asukile alilama na uchovu wa safari wanaokabiliwa wachezaji wenzake katika msimu wa Ligi, Asukile amesema ratiba ya Ligi inawabana wakati ameiomba TFF kuiangalia vizuri ratiba hiyo ili iendane sawa na Ligi pindi timu zinaposafiri mara kwa mara.

Kwa upande wao, Azam FC wameshindwa kuzungumza baada yakutoridhishwa na matokeo hayo. Hata hivyo Azam FC inafikisha alama 38 wakati Tanzania Prisons wenyewe wakipata alama 25.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...