NA TIGANYA VINCENT
HALMASHAURI ya Wilaya ya Kaliua imetoa shilingi milioni 10 za motisha na vyeti kwa shule za msingi na sekondari zilizofanya vizuri katika mitihani ya kitaifa.

Kauli hiyo imetolewa jana na Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kaliua Dkt. John Pima wakati wa kikao cha Baraza la Madiwani wa Halmashauri hiyo.

Alisema kuwa lengo la kutoa fedha hizo ni kutoa motisha kwa ajili ya kuwahamisha walimu waongeze juhudi ili kuondoa daraja sifuri na daraja la nne.

Dkt. Pima alisema motisha hiyo imezingatia shule zenye ufaulu kwa alama A, ufaulu wa somo kwa A na B pekee, shule zenye ufaulu wa wastani wa B na shule zenye ufaulu bila Daraja sifuri.

Alisema kuwa walipoanzisha mpango huo walianza na kutoa motisha jumla ya shilingi milioni 1 na sasa hivi wameamua kutoa milioni 10 na wanatarajia kuongeza hadi kufikia milioni 30.

Kwa upande wa Katibu Tawala Mkoa wa Tabora Msalika Makungu aliwataka walimu kuhakikisha wanaondoa Daraja sifuri na la nne mkoani humo.

Alisema sio jambo la kupendeza kuona kuwa mwalimu amekaa na mwanafunzi kwa kipindi cha miaka minne mwisho wake anapata daraja sifuri.

“Hata shule za Sekondari ambazo wanafunzi wanafanya vizuri walimu ni sawa na wao na wamesoma katika vyuo ambao nao wamesoma, hivyo hakuna sababu ya wanafunzi kufanya vibaya”alisema.
 Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Kaliua Dkt. John Pima  akijibu maswali ya papo kwa papo ya  Madiwani wakati wa kikao cha Baraza Madiwani kilichafanyika jana.
 Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Kaliua Dkt. John Pima  (kushoto) na Mbunge wa Jimbo la Kaliua Magdalena Sakaya (kulia) wakijadiliana jambo wakati wa kikao cha Baraza Madiwani kilichafanyika jana.
 Mwenyekiti wa Halmashauri ya Kaliua Haruna Kasele akiwasilisha taarifa ya utekelezaji wa mipango mbalimbali ya maendeleo wakati wa kikao cha Baraza la Madiwani kilichofanyika  jana.
 Katibu Tawala Mkoa wa Tabora Msalika Makungu akihutibia kikao  cha Baraza la Madiwani wa Halmashauri ya wilaya ya Kaliua kilichofanyika.
 Baadhi ya Madiwani, Walimu na wananchi wakiwa katika kikao cha Baraza la Madiwani wa Halmashauri ya Wilaya ya Kaliua jana ambacho pamoja na ajenda nyingine Baraza lilitoa fedha taslimu kwa Shule za Msingi na Sekondari zilizofanya vizuri katika mitihani ya kitaifa ya 2029. Picha na Tiganya Vincent.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...