Charles James, Michuzi TV

KATIKA kuhakikisha wanafunzi wa Jiji la Dodoma wanatumia teknolojia katika masomo yao, Mbunge wa Jimbo hilo Anthony Mavunde amekabidhi Vishkwambi 700 kwa shule 10 za jiji hilo.

Vishkwambi hivyo vimegaiwa kwa shule za msingi za serikali na binafsi ambapo kishkwambi kimoja kina gharama ya Sh Milioni Moja hivyo vyote jumla vikiwa na gharama ya Sh Milioni 700.

Akizungumza wakati wa kukabidhi vishkwambi hivyo, Mkuu wa Wilaya ya Dodoma Mhe Patrobas Katambi amempongeza Mavunde kwa kujitoa kuhakikisha vijana wanapata elimu bora na ya kisasa.

Amesema toka awe Mkuu wa Wilaya hiyo
ameshuhudia namna ambavyo Mavunde ametoa msaaasa mkubwa kwenye Jimbo hilo kwa kugusa kila sekta.

" Hakuna sehemu ambayo Mbunge hajagusa, wakina Mama wa Dodoma wamekua wakipata mikopo ya kutosha ambayo imekua msaada kwao kiuchumi.

Sekta ya afya ameigusa, Barabara za Jiji la Dodoma zinajengwa kwa kasi na hii lakini kwenye elimu amejenga shule na kukarabati majengo mengi ya shule za msingi na sekondari hakika wananachi wa Dodoma mna Mbunge makini sana," Amesema DC Katambi.

Kwa upande wake Mhe Mavunde amesema amegawa vishkwambi hivyo ili kuongeza chachu ya wanafunzi kufanya vizuri kwenye masomo yao pamoja na kurahisisha kazi ya ufundishaji kwa walimu.

Amesema ndoto yake kila siku ni kuona Jiji la Dodoma linapiga hatua kubwa kwenye elimu kwa kuzalisha vijana wengi wanaofaulu vizuri kwani anaamini kupata kwao elimu bora ndio njia ya wao kufanikiwa kwenye maisha na kuwa msaada kwa Taifa.

" Mhe DC kwa muda wote mimi nimekua nikiangaika kuboresha sekta ya elimu kwenye Jiji letu, na wala sifanyi hivyo kwa sababu nimekua Mbunge ninafanya hivi kwa mapenzi yangu na uchungu nilionao kwa vijana wetu wa Dodoma.

Tunashukuru Mhe Rais ametupa elimu bila malipo lakini hiyo haimaanishi sisi wengine hatuna wajibu tena, ni jukumu letu kumsaidia Rais kufikia azma yake ya kutoa elimu yenye viwango bora kwa watoto wa kitanzania," Amesema Mavunde.

Amewataka walimu na wanafunzi wa shule zilizopata vishkwambi hivyo kuvitunza kwa umakini ili viendelee kuwa msaada kwa watoto wengine kwa miaka mingi ijayo.

Mavunde amesema ataendelea kutoa vifaa hivyo kwa shule zingine katika awamu zijazo lengo ni kuhakikisha watoto wa Dodoma wanapata uelewa wa matumizi ya teknolojia wakiwa bado wadogo.

Akizungumza kwa niaba ya Chama cha Walimu Tanzania (CWT) Mkoa wa Dodoma, Katibu wa CWT Mkoa amemshukuru Mavunde kwa namna ambavyo amekua bega kwa bega na walimu katika kuwapatia motisha na kuwarahisishia kazi za ufundishaji.

" Hakika Mhe Mavunde umekua ni alama ya kiongozi kijana anaekwenda na wakati, uliwahi kutoa Kompyuta 78 kwenye shule zetu, umetoa misaada ya jezi, mipira na vifaa vingine vya michezo mashuleni kwa lengo la kukuza vipaji vya watoto wetu.

Siyo kwa wanafunzi tu hata kwa walimu umekua ukiwapa sapoti na motisha pale wanaposaidia ufaulu kuongezeka, tunakushukuru sana na zawadi yetu kwako ni cheti cha kutambua mchango wako kwetu na kukuahidi mabadiliko makubwa ya viwango vya ufaulu kwenye mitihani ijayo," Amesema..
 Mkuu wa Wilaya ya Dodoma, Patrobas Katambi na Mbunge wa Jimbo la Dodoma Mjini, Anthony Mavunde wakiwa katika picha ya pamoja na madiwani, walimu na wanafunzi baada ya kukabidhi vishkwambi 700 kwa shule 10 za msingi za Jiji hilo leo.
 Mkuu wa Wilaya ya Dodoma, Patrobas Katambi akizungumza na walimu, wanafunzi na wadau wa elimu wakati wa kukabidhi vishkwambi kwa shule 10 za jiji hilo.
 Mkuu wa Wilaya ya Dodoma, Patrobas Katambi akimkabidhi zawadi ya cheti Mbunge wa Jimbo la Dodoma Mjini, Anthony Mavunde leo cha kutambua mchango wake kwenye elimu. Cheti hicho kimeandaliwa na Chama Cha Walimu Jiji la Dodoma.
 Mbunge wa Jimbo la Dodoma Mjini, Anthony Mavunde akizungumza wakati wa ugawaji wa vishkwambi hivyo leo.
 Wanafunzi kutoka shule 10 za Jiji la Dodoma wakiwa na furaha wakati wa kukabidhiwa vishkwambi kwa ajili ya kujifunzia leo na Mbunge wa Jimbo la Dodoma Mjini, Anthony Mavunde

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...