Naibu Waziri wa Nishati, akipata
taarifa wa hali ya umeme ya Wilaya ya Liwale kutoka kwa Meneja Tanesco
wa Wilaya ya Liwale Festo Nhembo wakati akiwa kwenye ziara ya kazi ya
ukaguzi wa kazi ya usambazaji umeme.

Naibu Waziri wa Nishati,Subira
Mgalu,akiongea na wananchi wa kata ya Liwale mjini kabla ya kuwasha
umeme kwenye shule ya msingi ya kata hiyo, kulia Mkuu wa Wilaya ya
Liwale Sarah Vicent Chiwambwa.

Naibu waziri wa Nishati, Subira
Mgalu akifurahi pamoja na kina mama wa kijiji cha Makata, mara baada ya
kuwashwa kwa umeme kwenye zahanati ya kijiji hicho kilichopo kata ya
Makata,Wilaya wa Liwale Mkoa wa Lindi.

Wananchi wa kijiji cha Makata
wakimsikiliza Naibu waziri wa Nishati Subira Mgalu alipokuwa akihutubia
kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika kijijini humo wakati alipokuwa
kwenye ziara ya kazi ya ukaguzi wa kazi ya usambazaji umeme kijijini
humo.
*****************************
Hafsa Omar-LINDI
Naibu Waziri wa Nishati, Subira
Mgalu, amesema amefurahishwa na kuridhishwa na kasi ya uunganishwaji
umeme kwenye Taasisi za Umma zilizopo Wilayani Liwale kama Serikali
ilivyoagiza.
Ameyasema hayo,Februari
24,2020,kwa nyakati tofauti wakati akizungumza na wananchi wa Kata ya
Liwale mjini na wa kijiji cha Makata, Kata ya Makata, Wilaya ya Liwale,
Mkoa wa Lindi kabla ya kuwasha umeme kwenye Zahanati ya kijiji hicho na
kwenye ya Shule ya Msingi Naluleo.
Aidha, alisema ziara yake
hiyo,Mkoani humo lengo lake kukagua kazi za usambazaji umeme
zinavyoendelea katika Mkoa huo na pia kujionea mwenyewe kasi ya
usambazwaji wa umeme katika Taasisi za umma kama Serikali ilivyoagiza
zipelekewe umeme na amefurahishwa kuona shule na zahanati nyingi za
Wilaya hiyo zimeunganishwa na huduma hiyo.
“Rais Dkt.John Pombe Magufuli
aliagiza umeme huu tunavyoupeleka vijijini basi tunganishe kwenye
taasisi za umma hususani Shule,Zahanati, vituo vya afya,miradi ya maji,
ofisi za Serikali kwahiyo nimefurahi leo tunazindua kwenye shule ya
Msingi ambao Watoto wenu wanasoma hapa”Alisema.
Alisema, lengo la kupeleka umeme
kwenye Taasisi hizo, kuhakikisha kuwa huduma hizo zinazotolewa zinakuwa
za kiwango na zenye kukidhi mahitaji ya wananchi.
Alieleza kuwa, unganishwaji umeme
katika kwenye Shule ya kijiji hicho utaongeza ufaulu wa wanafunzi katika
shule hiyo,kwakuwa kutakuwa na kambi ya kujisome yenye uhakika wa
usalama kwasababu mwanga utapatikana muda wote katika shule hiyo na
wanafunzi kuweza kujisomea.
Vilevile, alisema kupatikana kwa
umeme kwenye Zahanati kwenye kata ya Makata itasaidia kuboresha huduma
za afya zinazotolewa kwenye zahanati hiyo ambapo huduma hizo zinatolewa
zitapatikana kwa muda wote na hakutakuwa na kisingizo cha kutotoa huduma
kwasababu ya giza.
Pia, aliwataka wananchi wa vijiji
hivyo wasitumie umeme kwa matumizi ya nyumbani, bali watumie umeme huo
katika kujiletea maendeleo kwa kujiajiri kwa kufanya shughuli mbalimbali
za kujipatia kipato.
“ Tumieni umeme kujiletea
maendeleo,kazi ya umeme ni pamoja na usalama majumbani,uboreshaji wa
huduma za afya,umeme unasaidia kukuza uchumi kwa mtu mmoja mmoja, na kwa
jamii kwa familia na Wilaya pia nataka Liwale iende mbali kiuchumi na
nawalika wawekezaji wakubwa na wadogo waje kuwekeza kwasababu kuna umeme
wa uhakika” Alisema.
Nae mbunge wa jimbo la Liwale,
Zuberi Kuchauka ameishukuru Serikali kwa kufanya kazi kubwa ya
usambazaji umeme nchini na kupeleke huduma hiyo kwenye wilaya humo na
kuahidi kuwa wananchi wa jimbo hilo watautumia umeme kwa matumizi sahihi
ambayo yatasaidia kujiletea maendeleo kwa mtu mmoja mmoja na kwa wilaya
pia.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...