Naibu Waziri wa Uchukuzi na
Mawasiliano, Mhandisi Atashasta Nditiye (aliyetangulia mbele katikati)
akipata maelezo kuhusu ukarabati wa vichwa vya treni kutoka kwa Kelvin
Kimario (wa kwanza kulia mbele), Meneja Msaidizi wa Karakana ya Reli,
Morogoro wakati wa ziara yake kwenye Karakana hiyo

Naibu Waziri wa Uchukuzi na
Mawasiliano, Mhandisi Atashasta Nditiye (wa nne kulia) akipata maelezo
kutoka kwa Mhandisi Albert Magandi, Mkurugenzi wa Uhandisi Mitambo
kuhusu utendaji kazi wa Karakana ya Reli, Morogoro wakati wa ziara yake
kwenye Karakana hiyo

Naibu Waziri wa Uchukuzi na
Mawasiliano, Mhandisi Atashasta Nditiye (wa kwanza kushoto) akipata
maelezo kuhusu utengenezaji wa vichwa vipya vya treni kutoka kwa
Mhandisi Wenceslaus Kamugisha, Meneja wa Mradi wa Kampuni ya SMH RAIL ya
Malaysia wakati wa ziara yake kwenye Karakana ya Reli, Morogoro

Naibu Waziri wa Uchukuzi na
Mawasiliano, Mhandisi Atashasta Nditiye akisisitiza jambo kwa viongozi
wa Karakana ya Reli, Morogoro wakati wa ziara yake kwenye Karakana hiyo

Naibu Waziri wa Uchukuzi na
Mawasiliano, Mhandisi Atashasta Nditiye (wa pili kulia) akipata maelezo
kuhusu ukarabati wa vichwa vya treni kutoka kwa Mhandisi Edgar Bakuza,
Meneja wa Karakana ya Reli, Morogoro wakati wa ziara yake kwenye
Karakana hiyo

Mafundi wa Karakana ya Reli,
Morogoro wakiendelea kukarabati vipuri vya vichwa vya treni wakati wa
ziara ya Naibu Waziri wa Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Atashasta
Nditiye (hayupo pichani) kwenye Karakana hiyo
…………………………………………………………………………………………………………
Na Mwandishi Wetu, Morogoro.
Naibu Waziri wa Uchukuzi na
Mawasiliano, Mhandisi Atashasta Nditiye amelielekeza Shirika la Reli
Tanzania (TRC) kununua vipuri kwa ajili ya kufanya matengenezo na
ukarabati wa vichwa vya treni kwa wakati
Nditiye ameyasema hayo wakati wa
ziara yake jana kwenye Karakana ya Reli Morogoro ambapo alikagua
matengenezo na ukarabati wa vichwa vya treni yanayoendelea kufanyika
kwenye karakana hiyo mkoani Morogoro
Pia, ameshuhudia utengenezaji wa
vichwa vipya saba vya treni unaofanywa na Kampuni ya SMH Rail ya kutoka
nchini Malaysia kwa kushirikiana na mafundi na wataalamu watanzania wa
karakana hiyo
Wakati akiwa ziarani hapo alifanya
kikao na viongozi na mafundi wa Karakana hiyo na kubaini kuwa TRC
inachukua muda mrefu kufanya manunuzi ya vipuri au oil kwa ajili ya
kukamilisha ukarabati au matengenezo ya vichwa vya treni ambapo manunuzi
yanachukua muda mrefu
“wataalamu wa manunuzi wa TRC
muache tabia ya kuchukua muda mrefu kufanya manunuzi ya vipuri au oil
kwa ajili ya kufanya matengenezzo au ukarabati wa vichwa vya treni, kama
kuna changamoto kwenye manunuzi au malipo, menejimenti ya TRC fanyieni
kazi jambo hili,” alisisitiza Nditiye
Aliongeza kuwa hatuhitaji tutafute
vipuri izidi miezi mitatu na fundi anaomba oil ili afanye matengenezo
ya kichwa cha treni inachukua miezi miwili kwa kuwa sisi Serikali ya
Awamu ya Tano inayoongozwa na Dkt. John Pombe Magufuli, Rais wa Jamhuri
ya Muungano wa Tanzania tumeona umuhimu wa reli, tutalinda reli yetu na
tutaendelea kurekebisha njia ili reli iendelee kuchagiza uchumi na
kuongeza pato la taifa letu kwa kuwa bila reli
kichwa cha treni
hakisogei na bila reli uchumi haupandi
Tunashukuru kwenye karakana hii
tuna mafundi na wataalamu wa kutosha ambao wako tayari kufanya kazi kwa
bidii na kujitolea ili kuhakikisha kuwa treni zetu zinatembea na reli
yetu inafanya kazi na wako tayari kufundisha vijana ili waweze
kuwaridhisha utaalamu huo
Naye Meneja wa Matengenezo ya
Vichwa vya Treni, Karakana ya Reli ya Morogoro, Mhandisi Edgar Bakuza
amekiri kuwepo kwa changamoto ya upatikanaji wa vipuri kwa wakati kwa
ajili ya kufanya matengenezo na ukarabati wa vichwa vya treni kwenye
Karakana hiyo
“Ni kweli changamoto za vipuri ni
kubwa, tunajitahidi kupambana nayo ndiyo maana tupo hapa kwa ajili ya
kuzikabili changamoto ambazo zinatukabili na natumai kutokana na
mashirikiano mazuri ambayo tunayo kati yetu sisi na viongozi wetu wa juu
changamoto hizo zinafanyiwa kazi na natumai mwisho wa siku sisi hapa
Morogoro huwa tunapimwa kutokana na uimara wa kazi tunazozifanya hasa
katika hivi vichwa vya treni, uimara wake pamoja na uwingi wao katika
hii fleet yetu ya locomotives katika hii reli ya kati, kwa hiyo tuko mbioni kuikabili na kuiondoa kabisa,” amefafanua Mhandisi Bakuza
Mhandisi Bakuza amesema kuwa
wanaendelea na matengenezo ya vichwa saba vya kupangia mabehewa na mradi
unaendelea vizuri na upo katika hatua nzuri ya kuweza kuukamilisha na
sasa kazi ya kuendelea kuunga vyuma na mabati mbali mbali inaendelea ili
kuweza kupokea vifaa mbali mbali ambavyo vimeagizwa nje ya nchi na
tayari vifaa vingi vimefika kwenye Karakana hiyo, vifaa vingine
vimeagizwa, vimesafirishwa na tayari vipo bandarini Dar es Salaam kwa
ajili ya kugombolewa na kufikishwa Morogoro
Ameongeza kuwa mradi huu
utakapokamilika utawezesha kuondoa vichwa vikubwa vya treni kutoka
katika kazi ya kupangia mabehewa ili vitumike katika kazi ya kuvuta
mzigo mkubwa kwenda mikoa ya bara
Vichwa vinavyotengenezwa vitakuwa
na kazi ya kuvuta mzigo kutoka Bandari ya Dar es Salaam ili kuufikisha
Bandari ya TRC iliyopo eneo la Kwala mkoani Pwani ili mabehewa hayo
yavutwe na kichwa kikubwa cha treni kuelekea bara
Naye Mkurugenzi wa Utawala na
Rasilimali Watu wa TRC, Halima Lumuli alikiri uwepo wa changamoto hiyo
ya upatikanaji wa vipuri ila watajitahidi kuhakikisha vinapatikana kwa
kuwa vichwa vya treni ndio kila kitu katika utendaji wa TRC na Shirika
litajitahidi kuboresha eneo hilo pamoja na kuboresha maslahi ya
watumishi na kuwapatia mafundi mafunzo ya kuongeza uwezo na weledi ili
utendaji kazi wao uweze kuongeza mapato ya Shirika
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...