Balozi wa Tanzania nchini Ufaransa, Mhe. Samwel Shelukindo (katikati) akiwa kwenye picha ya pamoja na Ujumbe wa Tanzania unaoshiriki kwa mara ya kwanza katika Maonesho ya Kimataifa ya Bidhaa za Kilimo ya Paris yanayofanyika mjini humo kuanzia tarehe 22 Februari 2020 hadi tarehe 1 Machi 2020.
Wageni mbalimbali wakipata maelezo kuhusu fursa za bidhaa za kilimo zinazopatikana Tanzania walipotembelea Banda la la Tanzania wakati wa Maonesho ya Kimataifa ya Bidhaa za Kilimo yanayofanyika jijini Paris kuanzia tarehe 22 Februari 2020 hadi tarehe 1 Machi 2020.

************************

Tanzania inashiriki kwa mara ya kwanza katika Maonesho ya Kimataifa ya Bidhaa za Kilimo ya Paris 2020 yanayofanyika jijini Paris, Ufaransa kuanzia tarehe 22 Februari 2020 hadi tarehe 1 Machi 2020.

Maonesho hayo ambayo yalifunguliwa na Mhe. Rais Emmanuel Macron wa Ufaransa, yanatarajiwakutembelewa na zaidi ya watu 600,000.

Wakati wa maonesho hayo, Tanzania itapata fursa ya kuonyesha bidhaa zake yakiwemo mazao ya kimkakati. Ujumbe wa Tanzania katika maonyesho hayo unaongozwa na Bw. Victor Rugemalila kutoka TANTRADE.

Ubalozi wa Tanzania ambao unaratibu maonesho hayo kupitia Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, unaishukuru Kampuni ya Tanzania Re-assurance (TAN-RE) ya Dar es Salaam, Tanzania, kwa kufadhili kwa kiasi kikubwa ushiriki wa Tanzania katika maonyesho. Aidha, Ubalozi unatambua mchango wa Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB) na Kampuni ya Kahawa ya Inter State.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...