1. UWANJA


Kwa kawaida uwanja wa mpira Wa miguu huwa na Urefu Wa mita 100  –  120  na Upana Wa mita  50 – 60 . Kwa kawaida Uwanja Wa mpira Wa miguu Una alama za mistari ambazo ni pamoja na


– Mstari mrefu pembeni mwa Uwanja Unaoashiria mwisho Wa Uwanja .

 – Mstari mrefu Wa Katikati Unaogawa Uwanja katika pande 2 Zilizolingana .katikati ya Uwanja kuna mduara wenye nusu kipenyo cha mita 9.15.

 – Mstari mrefu Upande Wa goli Unaoashiria mwisho Wa Uwanja upande Wa goli .

 – Pia kuna nusu duara katika makutania ya Mstari Wa pembeni na Mstari Wa goli ambapo huitwa Kona .

 2. MPIRA

 Mpira Wa miguu unaweza kutengenezwa kwa kutumia Ngozi , plastiki , au makunzi mengine yanayofaa . Kwa kawaida mpira Wa miguu huwa na kipenyo cha sm 68 – 70 na Uzito Wa gramu 410 – 450 na Ujazo Wa 1.1 – 1.6  .


– Utofauti Wa Kipenyo na Uzito Wa mpira Wa miguu hutegemea Uwezo ama rika la mchezaji au watumiaji .


3. IDADI YA WACHEZAJI

Mpira Wa miguu huchezwa na wachezaji 22 maana ya wachezaji 11 Kwa kila timu , Wachezaji Wa akiba wanaoruhusiwa ni 7 na kati ya hao wanaoruhusiwa kucheza ni wachezaji watatu (3) tu .

Katika mashindano ambayo hayatambuliwi na FIFA Idadi ya wachezaji Wa akiba inategemeana na makubaliano ya timu 2 husika .

4. VIFAA VYA MICHEZO

Vifaa vya michezo ni muhimu katika mchezo Wa mpira Wa miguu , kwa kawaida mpira Wa miguu unahitaji vifaa kama vile  Sare ambazo hazifanani na timu pinzani wala mwamuzi Wa mchezo na walinda milango , Viatu , soksi , Kitambulisho/Kitambaa cha Unahodha , Filimbi , Daftari la kutunzia Kumbukumbu za mchezo , Saa , Kadi ya Njano na Nyekundu  , Pia na Ubao Unaotumika kubadilishia wachezaji , Kibendera Kwaajili ya Waamuzi wasaidizi na Nyavu za magoli .


5. MWAMUZI

– Mwamuzi ndiye anayeongoza mchezo na Kutafsiri sheria wakati Wa mchezo .Hutoa maamuzi ndani ya Kipindi cha mchezo na kutoa taarifa ya mchezo husika .

  Ndiye msemaji au mwamuzi Wa mwisho Pale inapobainika kwamba Sheria ya mchezo imekiukwa kwa namna yeyote ili ikiwa ni pamoja na kutoa adhabu pindi mchezaji anapofanya Kosa ndani ya Uwanja .


6.  WAAMUZI WASAIDIZI


Hawa ni Watendaji wengine wanaomsaidia mwamuzi Wa katikati wakati mchezo unaendelea .


– Humsaidia mwamuzi mkuu kuhusu matukio yanayotendeka nje na ndani ya Uwanja .

– Idadi ya waamuzi wasaidizi Hutegemea mashindano au mchezo husika , Waamuzi hao hutambulika kama washika vibendera Namba 1&2 na Kamisaa Wa mchezo anayetunza kumbu kumbu . Pia mashindano mengine huruhusu waamuzi wakae nyuma ya goli mfano UEFA CHAMPIONS LEAGUE .


7. MUDA

 Kwa kawaida mpira Wa miguu huchezwa kwa dakika 90′ katika Vipindi 2 Yaani dk 45′ Kwa kila kipindi , Baada ya dakika 45 za kipindi cha kwanza cha mchezo mchezo husimama ( mapumziko) kwa muda Usiopungua dk 10 na Usiozidi 15 .

 Pia , Kama muda Wa nyongeza dk 30′ Utaongezwa kwa Lengo la kumpata mshindi , timu zitapumzika kwa dk 5′ tu baada ya dk 15′ Wa kipindi cha kwanza katika dk 30 za nyongeza ( Extra time ) na kipenyo kisha kubadilishana magoli tayari kwa kumalizia kipindi cha 2 . Ila muda waweza kupunguzwa kwa makubaliano ya timu husika .

 8.  KUANZA NA KUANZISHWA TENA MCHEZO

 Mpira huanzishwa kwa timu 1 kucheza mpira baada ya mwamuzi kuruhusu mchezo kuanza .

 – Mchezo huanzishwa tena baada ya goli kufungwa na baada ya kosa kutendeka na mwamuzi akapuliza Filimbi au kama mpira ukatoka nje au mchezaji kuumia N.K

 9. MPIRA KUWA NJE NA NDANI YA UWANJA

 Mpira Utakuwa nje ya mchezo kama mpira Utatoka nje ya Uwanja na pia baada ya goli kufungwa .

 Na pia , mpira Utakuwa ndani ya mchezo kama uko ndani ya Uwanja na Unaendelea Kuchezwa .

 10.  NAMNA YA KUFUNGA GOLI

 Katika mchezo Wa mpira Wa miguu , goli litahesabiwa kama mpira utavuka Mstari wa goli na kuingia katika eneo la wavu kwa Kufungwa au Kujifunga .


Pia goli litahesabiwa kama mpira Litavuka Mstari chini ya Uwanja au Ukiwa hewani na Likaonekana Ukavuka Mstari Wa goli .


11. KUOTEAKUOTEA Ni kitendo cha mchezaji kuzidi au kupokea mpira akiwa mbele ya wachezaji wote Wa timu pinzani na akiwa ndani ya Eneo la timu pinzani .


– Mchezaji anaweza akawa katika nafasi ya kuotea lakini asitafsiriwe kama ameotea kama Hajajishughulisha kabisa na mpira .– Dhana ya kuotea hutegemea mambo matatu muhimu ambayo ni Nafasi , kucheza na Kutoa .– Pia mchezaji hatakuwa ameotea ikiwa walinzi Wa timu pinzani Watamkimbia au kutojishughulisha kabisa pale mchezaji Wa timu pinzani atakapo pokea mpira na kufunga goli .– Mchezaji Hatatafsiriwa kama ameotea akiwa amepasiwa na mchezaji wa timu pinzani kwa Kujua au Kutojua .– pia , Ikiwa mchezaji yuko katika nafasi ya kuotea na mwenzake mwenye mpira akapiga mpira golini moja kwa moja bila kumpasia mpira huyo aliyeko katika nafasi ya kuotoa na kufunga goli , hapo mwamuzi attaruhusu goli bila kutafsiri Kuotea .– Mchezaji atakuwa ameotea Iwapo mpira Utapigwa golini Ukagonga mlingoti mojawapo Wa goli au mlinda mlango na kurudi ndani ya Uwanja na kuguswa na mchezaji aliyekuwa katika nafasi ya Kuotea .– Aidha , Hakutakuwa na dhana ya kuotea pale mchezaji atakapokutana na mpira Uliochezwa na mlinda mlango .– Mpira Wa kurushwa Hauna kuotea , Pia mchezaji hatakuwa ameotea endapo atapokea mpira katika eneo lake kabla hajavuka Mstari Wa katikati ya Uwanja .12. MAKOSA YA UTOVU WA NIDHAMUNi kutenda jambo ambalo lililo nje ya kanuni za kimchezo Wa mpira Wa miguu au kuonyesha tukio lisilo la Kiungwana pale mchezaji anapokuwa nje au ndani ya Uwanja .Makosa atendayo mchezaji anaweza kuonywa kwa kadi ya Njano au Nyekundu na kutolewa nje ya Uwanja . kwa kawaida makosa yanayoonywa kwa kadi ya manjano ni kama Vile kushika na Kuunawa mpira bila kukusudia  , Kumsukuma mchezaji Wa timu pinzani katika hali ya kutaka kuchukua mpira , Kupoteza muda , Kumvuta au kumshika mchezaji Wa timu pinzani wakiwa katika hali ya kucheza mpira .Makosa ya kadi nyekundu ni kama vile , Kutukana , Kupigana , Kucheza rafu kwa nyuma , Kukaba kwa nguvu kwa kunyoosha miguu mmoja au yote miwili mbele wakati mchezaji mwingine anataka kupokea mpira au kucheza N.KKwa mujibu Wa sheria hii– Mchezaji atakayeonyeshwa kadivnyekundu ya moja kwa moja atakosa mechi 3– Mchezaji atakayeonywa kwa kadi ya njano 2 katika mchezo mmoja atatolewa kwa kadi nyekundu na kukosa mchezo 1 .– Mchezaji akionyeshwa kadi za njano katika michezo 5 ndani la Ligi 1 au mashindano atakosa mechi 1 , kadi 10 atakosa michezo 2 na kadi 15 atakosa michezo 3 .– Endapo mchezaji atafikisha kadi za njano 20 katika msimu mmoja , basi kamati ya maadili ya wachezaji itakaa na kuamua adhabu kwa mchezaji huyo .13. PIGO HURUNi hali ya mwamuzi Wa michezo kuamuru mpira upigwe kuelekea upande Wa timu ya mtenda makosa .– Wakati mpira Unapigwa golini , Wachezaji wengine wanatakiwa kuwa katika Umbali Usiopungua mita 9.15 au hatua zisizopungua 10 kutoka pale mpira Ulipo .14 . PIGO LA PENATINi kitendo cha mpira kutengwa kwenye Kisanduku cha meta 12 kutoka goli .Pigo la penati linawahusisha wachezaji wawili tu , mpigaji na mlinda mlango na wachezaji wengine wrote wanatakiwa kuwa nje ya 18 .Kuna aina 2 za pigo la penati ambazo ni , Penati ndani ya muda Wa mchezo yaani ndani ya dk 90′ na pigo la penati baada ya muda Wa mchezo ambalo linalenga kutafuta mshindi Wa mchezo Mara baada ya timu zote kutoshana nguvu ndani ya dakika za mchezo.

 Mpiga penati ndani ya muda Wa mchezo hufanya mambo mawili ambayo ni Kupiga mpira golini 1 kwa 1 au kumtengea mwenzake aliye nje ya 18 ….mfano mzuri ni Lionel messi na Luis Suarez msimu Wa 2015/2016

– Mpigaji Wa penati  anaruhusiwa kuucheza tena mpira  uliorudi ndani ya Uwanja baada ya mlinda mlango kuucheza na hatoruhusiwa kuucheza endaoo Utagonga mlingoti na kurudi Uwanjani .15. MPIRA WA KURUSHA


Hutokea pale ambapo timu pinzani watakapokuwa wameutoa .


Hauhusiani na GoaL Kick , na Utarushwa kuelekea katika Lango la aliyeutoa .

16 . PIGO LA GOLI

 Hiii ni GoaL Kiki , Hutokea endapo timu shambulizi ikatoa au kupaisha Juu au pembeni ya Lango shambuliwa .17. PIGO LA KONA


Baada ya timu shambuliwa kutoa katika Mstari Wa goli alishi , timu shambulia hupewa nafasi ya Kupiga Pigo la kona katika timu pinzani ( shambuliwa ) .


Katika upigaji Wa kona mchezaji anaweza kupiga moja kwa moja au kuanza kwa Kupasia .

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...