ECOBANK Tanzania imeshiriki mbio za Kilimanjaro Marathon kwa mwaka 2020 na kushiriki katika ukimbiaji wa mbio za Marathoni za kilomita 42.2 na mbio za nusu Marathoni za kilomita 21.1.
Katika mbio hizo mshiriki kutoka Ecobank Tanzania Tusekile Mwakyembe
aliibuka kinara kwa kumaliza kukimbia mbio za kilomita 42.2 akitumia
masaa matani na dakika 27 pekee.
Katika hafla hiyo iliyohudhuriwa
na Waziri mwenye dhamana ya utalii Dkt. Hamis Kigwangala amewapongeza
washiriki na kuwashukuru waandaji wa mbio hizo ambazo zimejumuisha
washiriki zaidi ya elfu kumi na mbili (12,000) kutoka nchi zaidi ya 56.
Amesema
ujio wa wageni hao kutoka mataifa mbalimbali ni fursa ya kiuchumi kwa
Watanzania pia ni moja ya mkakati wa kukuza na kutangaza vivutio
mbalimbali vya Utalii.



Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...