Waziri wa wa Mambo ya Nje wa Nepal, Mhe. Pradeep Gyawali alifungua rasmi ofisi ya Mwakilishi wa Heshima wa Tanzania nchini Nepal katika hafla iliyofanyika katika Hoteli ya Radisson Jijini Kathmandu tarehe 02 Machi 2020.

Katika hotuba yake, Waziri Gyawali alieleza kuridhishwa kwake kutokana na uhusiano thabiti wa kidiplomasia uliopo kati ya nchi hizi mbili ambapo zinashirikiana na kujenga hoja zinazofanana kwenye medani ya Umoja wa Mataifa, Umoja wa Nchi Zisizofungamana na Upande Wowote, Kundi la 77 na nyinginezo.

Hata hivyo, Waziri Gyawali alielezea umati wa washiriki katika hafla hiyo kuwa kwa sasa, uhusiano huu unapaswa kujikita zaidi katika maeneo ambayo mbia mmojawapo anaweza kunufaika na ujuzi na uzoefu kutoka kwa mwenzake. Akataja maeneo ambayo Nepal imefanikiwa zaidi kama vile utalii wa kupanda milima ambapo Nepal inavyo vilele vya milima nane mirefu kuliko yote duniani ikiongozwa na Mlima Everest.

Awali akimkaribisha Mheshimiwa Waziri Gyawali, Balozi Baraka Luvanda anayeiwakilisha Tanzania nchini India na Nepal alielezea juu ya umuhimu wa ofisi ya Mwakilishi wa Heshima kuwa itasaidia kutoa huduma za Kikonseli kwa karibu zaidi na pia itasaidia kuimarisha uhusiano baina ya nchi hizi mbili.

Balozi Luvanda alitaja maeneo ambayo yanaweza kutazamwa kama ya kuanzia kama vile (i) Kuwa na Makubaliano ya Mashauriano ya Kisiasa (Political Consultations) (ii) Kuwa na Makubaliano katika Sekta ya Usafiri wa Anga (Bilateral Air Services) ambapo “Air Tanzania” inaweza kuingia ubia na “Nepal Airline” (iii) Kuwa na Makubaliano kwenye sekta ambazo Nepal inafanya vizuri kama vile Utalii wa kupanda milima na Kilimo.

Bwana Rajesh Chaudhary, raia wa Nepal amekwishaanza rasmi kazi ya Uwakilishi wa Heshima baada ya kukamilika kwa taratibu zote za kidiplomasia.
Waziri wa Mambo ya Nje wa Nepal, Mhe. Pradeep Gyawali akizungumza katika hafla ya ufunguzi rasmi wa ofisi ya Mwakilishi wa Heshima wa Tanzania nchini Nepal iliyofanyika katika Hoteli ya Radisson Jijini Kathmandu, Nepal tarehe 02 Machi 2020.
Balozi wa Tanzania nchini India na Nepal, Mhe. Baraka Luvanda akihutubia wageni waalikwa (hawapo pichani) wakati wa hafla ya ufunguzi rasmi wa ofisi ya Mwakilishi wa Heshima wa Tanzania nchini Nepal iliyofanyika katika Hoteli ya Radisson Jijini Kathmandu, Nepal tarehe 02 Machi 2020.
Mwakilishi wa Heshima wa Tanzania nchini Nepal Bwana Rajesh Chaudhary akihutubia katika hafla ya ufunguzi rasmi wa ofisi ya Mwakilishi wa Heshima wa Tanzania nchini Nepal iliyofanyika katika Hoteli ya Radisson Jijini Kathmandu, Nepal tarehe 02 Machi 2020.
Balozi wa Tanzania nchini India na Nepal, Mhe. Baraka Luvanda (wa pili kulia) akiwa katika picha ya pamoja na Waziri wa Mambo ya Nje wa Nepal, Mhe. Pradeep Gyawali (wa pili kushoto), Mwakilishi wa Heshima wa Tanzania nchini Nepal, Bwana Rajesh Chaudhary (wa kwanza kulia) na Mkuu wa Wawakilishi wa Heshima mjini Kathmandu, Nepal, Bwana Pradeep Kumar Shrestha katika hafla ya ufunguzi rasmi wa ofisi ya Mwakilishi wa Heshima wa Tanzania nchini Nepal iliyofanyika katika Hoteli ya Radisson Jijini Kathmandu, Nepal tarehe 02 Machi 2020.
Balozi wa Tanzania nchini India na Nepal, Mhe. Baraka Luvanda (wa pili kulia) akimkabidhi zawadi rasmi ya kitanzania-picha ya tingatinga Waziri wa Mambo ya Nje wa Nepal, Mhe. Pradeep Gyawali katika hafla ya ufunguzi rasmi wa ofisi ya Mwakilishi wa Heshima wa Tanzania nchini Nepal iliyofanyika katika Hoteli ya Radisson Jijini Kathmandu, Nepal tarehe 02 Machi 2020.
Baadhi ya Wawakilishi wa Heshima wa nchi mbalimbali mjini Kathmandu, Nepal wakiwa kwenye hafla ya ufunguzi rasmi wa ofisi ya Mwakilishi wa Heshima wa Tanzania nchini Nepal iliyofanyika katika Hoteli ya Radisson Jijini Kathmandu, Nepal tarehe 02 Machi 2020.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...