Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha kupambana na vitendo vya ukatili wa Kijinsia (CAGBV), Sophia Komba, ambaye pia ni Mjumbe wa Bodi ya LHRC akiongea na Vyombo vya habari katika kikao hicho kilichowakutanisha wadau wa haki za binadamu ili kuupitia mkataba wa Afrika unaohusu demokrasia, uchaguzi , utawala bora na haki za binadamu kwa lengo la kuweka mikakati ya kushawishi serikali iweze kuuridhia. Mkutano huo ulifanyika Dodoma mapema leo.

Afisa Programu na Mratibu wa Ofisi Dodoma wa Kituo Sheria na Haki za Binadamu (LHRC), William Mtwazi akiongea katika kikao kilichowakutanisha wadau wa haki za binadamu ili kuupitia mkataba wa Afrika unaohusu demokrasia, uchaguzi , utawala bora na haki za binadamu kwa lengo la kuweka mikakati ya kushawishi serikali iweze kuuridhia. Mkutano huo ulifanyika Dodoma mapema leo.


Mkurugenzi wa Women Wake Up (WOWAP) ambaye pia ni Mbunge wa Viti maalum, Fatma Toufiq akiongea katika kikao hicho kilichowakutanisha wadau wa haki za binadamu ili kuupitia mkataba wa Afrika unaohusu demokrasia, uchaguzi , utawala bora na haki za binadamu kwa lengo la kuweka mikakati ya kushawishi serikali iweze kuuridhia. Mkutano huo ulifanyika Dodoma mapema leo.


………………………………………………………………
Na Mwandishi wetu,

Wadau wa haki za binadamu wamekutana leo jijini Dodoma kujadili Mkataba wa Afrika kuhusu Demokrasi, Uchaguzi na Utawala Bora kwa lengo la kuweka namna bora ya kushawishi watunga sera waweze kuukubali na kuuridhia ili utumike katika sheria za nchi.

Akiongea katika kikao kazi cha siku moja kilichoandaliwa na Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC), Afisa Programu na Mratibu wa Ofisi ya Dodoma wa Kituo hicho cha sheria, William MtwaziMalisem kuwa lengo la kikao kazi hicho ni kuwakutanisha wadau wa haki za binadamu ili kuupitia mkataba huo wa Afrika na kuangalia yaliyomo katika mkataba waweze kuielimisha jamii kuhusu mkataba huo ili nao waweze kupaza sauti zao kwa watunga sera na serikali iweze kuuridhia.

“Kati ya nchi wanachama 55 wa Umoja wa Afrika ni nchi tisa tu ambazo hazijaridhia mkataba huo kutumika katika sheria zao, moja ya nchi hizo ni Tanzania, hivyo tumekutana hapa kujadiliana na kujaribu kuangalia kwa nini mpaka sasa mkataba huu haijauridhiwa, shida iko wapi na kutafuta namna bora ya kushawishi watunga sera kuweza kuukubali”, alisema Mtwazi

Aliendelea kusema kuwa watakapokuwa wanaupitia mkataba huo utawasaidia kujua umuhimu wake na kupima uchaguzi uliopita ulikuwa mzuri kiasi gani na wapi inabidi paboreshwe zaidi ili uchaguzi uwe mzuri zaidi.

“Hii ni hatua ya kwanza ambapo wadau tumekutana kuujadili mkataba kuuelewa vizuri , hatua itakayofata ni kukutana na mamlaka husika kama Kamati ya Kudumu ya Katiba na Sheria ya Bunge, Wizara ya Katiba na Sheria, Wizara ya Mambo ya Nje na wadau wengine ili kuzishawishi kuukubali na kuridhia uingizwe katika sheria zetu”, aliongeza Mtwazi

Mkataba huo wa Afrika kuhusu Demokrasia, Uchaguzi na Utawala bora ulitungwa mwaka 2007 katika mkutano mkuu wa Umoja wa Afrika (AU) na kuanza kutumika mwaka 2012 baada ya nchi kumi na tano (15) kuuridhia kama mkataba huo unavyohitaji.

Mkataba huu unasisitiza nchi wanachama kuwa na taasisi inayosimamia uchaguzi ambao ni huru, haki, usawa na kwa uwazi ili kujenga utamaduni wa kubadilishana uongozi kwa salama na amani.

Aidha, Mkataba huo unahimiza umuhimu wa nchi wanachama kuwa na mifumo ya kujipima kila baada ya uchaguzi ili kuangalia mapungufu kwa lengo la kuboresha ili kuwa na uchaguzi mzuri zaidi.

Mpaka sasa kando ya Tanzania, nchi nyingine ambazo bado hazijaridhia ni pamoja na Kameruni, Morocco, Libya, Visiwa vya Shelisheli, Misri, Zimbabwe na Gambia.

Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha kupambana na vitendo vya ukatili wa kijinsia (CAGBV), Sophia Komba alisema kuwa mkataba huu ukiridhiwa utaweka njia ya kuongoza kupata uchaguzi huru na wa haki kwa sababu unasisitiza masuala ya demokrasia, haki za binadamu na utawala bora.

Komba alisema kwa kuwa Tanzania inatarajia kufanya uchaguzi mkuu hivyo anaona ni muhimu kusisitiza umuhimu wa kuwa na uchaguzi huru na wa haki nchini ili demokrasia iweze kuimarika.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...