Wafungwa 150 kutoka katika Mikoa ya Mwanza, Shinyanga na Tabora wamepelekwa katika Gereza la Kwitanga Mkoani Kigoma ikiwa ni mkakati maalumu wa Serikali kuliteua gereza hilo kuwa Kituo Kikuu cha Uzalishaji wa zao la mchikichi nchini.
Hayo yamesemwa leo na Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni wakati wa ziara ya kukagua maendeleo ya mkakati huo uliotolewa maagizo na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa katikati ya mwaka 2018 alipofanya ziara gerezani hapo ukiwa na lengo la kulifanya Jeshi la Magereza kuingia katika mfumo wa uzalishaji mali.
“Katika kutekeleza agizo la Waziri Mkuu Kassim Majaliwa ambalo ni agizo la serikali, wizara tumeongeza nguvukazi hapa kwa kuleta wafungwa 150 na muda si mrefu tutaongeza wafungwa wengine 300 kutoka magereza mbalimbali nchini ili kuweza kuongeza uzalishaji huku eneo lenye ukubwa wa ekari 6000 linatarajiwa kulimwa zao hilo sambamba na kusambaza mbegu zinazozalishwa gerezani hapo kwenda Halmashauri za Mikoa, Taasisi za Umma, Asasi za Kiraia na Sekta Binafsi,” alisema Masauni
“Lakini pia ili kuliwezesha gereza hili tumeliagiza Shirika la Uzalishaji Mali la Jeshi la Magereza kulichukua Gereza la Kwitanga na kuliingiza katika kundi la magereza yanayowezeshwa na shirika ili kuweza kutatuliwa matatizo yao ya kifedha badala ya kusubiri bajeti kuu kutoka serikalini ambayo inakua haitoshi.
Akizungumza katika ziara hiyo, Mkuu wa Magereza mkoani Kigoma, Kamishna Msaidizi Leonard Bushiri aliunga mkono hoja ya Gereza Kwitanga kuchukuliwa na Shirika la Uzalishaji Mali huku akikiri baadhi ya masuala kukwama kutokana na changamoto za kibajeti.
“Nafikiri hili suala la gereza kuchukuliwa na Shirika la Uzalishaji Mali litatatua changamoto nyingi za kibajeti na kiuendeshaji maana gereza halina gari kubwa kwa ajili ya uvunajina usafirishaji wa mafuta kutoka gerezani kwenda kwa mtumiaji, hakuna bajeti ya uendeshaji kwa mfano kukamua lita 100 mpaka 120 za mafuta tunahitaji maji lita 1000 hivyo fedha kwa ajili ya kununulia umeme ili kusukuma maji ni changamoto, kwahiyo kuingizwa kwenye shirika itasaidia changamoto nyingi” alisema ACP Bushiri
Sambamba na kulima zao la mchikichi Gereza Kwitanga linalima pia mahindi, mpunga, mihogo, maharage na Bustani za mbogamboga.

Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (wapili
kulia) na Mkuu wa Gereza Kwitanga, Mrakibu Mwandamizi, Dominick Kazmil
wakiangalia matunda ya mchikichi yaliyovunwa katika gereza hilo ikiwa ni
utekelezaji wa agizo la Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa kutaka Gereza la
Kwitanga lililopo wilayani Kigoma kuwa Kituo Kikuu cha Uzalishaji wa
zao la Mchikichi nchini ikiwa ni mkakati maalumu wa kufufua kilimo cha
zao hilo.Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (watatu
mstari wa mbele) akimsikiliza Mkuu wa Gereza Kwitanga, Mrakibu
Mwandamizi, Dominick Kazmil baada ya kuangalia miche ya michikichi
iliyooteshwa katika gereza hilo ikiwa ni utekelezaji wa agizo la Waziri
Mkuu, Kassim Majaliwa kutaka Gereza la Kwitanga lililopo wilayani
Kigoma kuwa Kituo Kikuu cha Uzalishaji wa zao la Mchikichi nchini
ikiwa ni mkakati maalumu wa kufufua kilimo cha zao hilo.Wengine ni
ujumbe uliofuatana na Naibu Waziri.
Matunda ya Mchikichi yaliyovunwa katika mashamba ya Gereza Kitwanga
yakiwa yameanikwa juani tayari kwa kukamuliwa mafuta ikiwa ni
utekelezaji wa agizo la Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa kutaka Gereza hilo
lililopo wilayani Kigoma kuwa Kituo Kikuu cha Uzalishaji wa zao la
Mchikichi nchini ikiwa ni mkakati maalumu wa kufufua kilimo cha zao
hilo.

Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni akiangalia mpango kazi wa kilimo cha mchikichi katika Gereza la Kwitanga ikiwa ni ufuatiliaji wa utekelezaji wa agizo la Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa kutaka Gereza hilo lililopo wilayani Kigoma kuwa Kituo Kikuu cha Uzalishaji wa zao la Mchikichi nchini ikiwa ni mkakati maalumu wa kufufua kilimo cha zao hilo,Kushoto ni Mkuu wa Gereza Mrakibu Mwandamizi, Dominick Kazmil na Kulia ni Mkuu wa Magereza Kigoma Kamishna Msaidizi Leonard Bushiri.Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...