Charles James, Michuzi TV

KATIKA kuunga mkono jitihada zinazofanywa na serikali kwenye mapambano ya kuzuia maambukizi ya ugonjwa wa Corona, Mashirika yasiyo ya kiserikali (AZAKI) yamechangia Sh Milioni 79 kwa kamati ya kupambana na ugonjwa huo inayoongozwa na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa.

AZAKI pia imeahidi kutoa elimu kwa jamii kuhusu jinsi ya kujikinga na ugonjwa huo ikiwemo kuhamasisha wananchi kutumia vitakasa mikono, maji ya kunawa, kuepuka misongamano isiyo ya lazima na kuwahi kituo cha afya pale wanapoona dalili za ugonjwa huo.

Akizungumzia mbele ya waandishi wa habari leo  jijini Dodoma  baada ya kukabidhi mchango wao  kwa Mwenyekiti Wa Kamati ya kupambana na Corona Waziri Mkuu Kassim Majaliwa ,Rais wa Foundation for Civil Society Dkt Stigmata Tenga amesema kwa kutambua umuhimu wa Jambo hilo na kwakuunga mkono Serikali wametoa shilingi Milioni 79 na kutoa ahadi ya kutoa elimu.

Dk Stigimata amesema wameamua kuungana na serikali katika mapambano ya ugonjwa huo kwa kutambua kuwa taasisi na mashirika yao kwa namna moja ama nyingine wamekua na mahusiano ya moja kwa moja na wananchi ambao ndio nao ni wahanga wa ugonjwa huo.

Pia amesema wanafanya hivyo kwa maana ya kutoa mchango kwa ajili ya mkakati huo wa kitaifa wa kupambana na Corona ambapo sehemu ya  mashirika ikiwamo  TWAWEZA, TAULA ,TGNP,na mashirika mengine wamejikusanya na kupeleka mchanga wao ili iweze kusaidia.

" Tutaendelea kuhamasisha jamii kwa maana kuweza kuwa pamoja kwani Jambo hili si la mtu mmoja ni la wengi licha ya sisi kufanya hivi lakini tunaomba  makundi mengine na yenyewe kujitokeza.

Ndugu zangu wanahabari niwasihi kuendelea kuhamasisha wananchi wetu kufuata maelekezo ambayo yamekua yakitolewa na wataalam wa afya na viongozi wetu, kwa pamoja tuungane dhidi ya adui wetu ambaye ni Corona"amesema.

Nae Mkurugenzi mtendaji wa Chama Cha wanasheria wanawake (TAWLA), Tike Mwambipile amesema wanatambua ni kwa kiasi ugonjwa huo una madhara kwa wanawake na watoto hivyo wakaona ni vema nao waungane na serikali kusaidia mapambano hayo.

" Makundi ya wanawake, watu wenye ulemavu na watoto wanafanya kazi ndogondogo nyingi sana sasa kwa sasa hali ni mbaya hivyo tunafahamu wameathirika kiuchumi, sasa kwa hiki kidogo tulichojaliwa tumeona nao tuwaguse," Amesema Mwambipile.

Amesema makundi Kama wanawake ,watoto ma hata wenye ulemavu wao  wanafanya kazi ndogondogo  nyingi ambazo kwa Sasa zimepungua Sana na hivyo kwa kutambua hilo wameamua kuchangia kidogo ili wanawake na familia zao waweze kupata kidogo.

Kwa upande wake Mkurugenzi kutoka shirika la LSF Lulu Ngwanakilala amesema wamekua Karibu na serikali kama wadau wengine katika kuisaidia kutoa michango ili kupambana na Corona.

Lulu amesema wao ni wadau wakubwa wa serikali kwani wamekua wakifanya kazi nyingi za kuisaidia haki za makundi yenye uhitaji wa kisheria hivyo katika jambo hili la Corona pia wameguswa kuchangia na kushirikiana na serikali kwenye mapambano ya ugonjwa huo.

" Kama ambavyo tumekua wadau wa serikali kwenye nyanja nyingine basi na katika hili hatujataka kuwa nyuma, tumeona umuhimu wa kuweka nguvu zetu na kuhakikisha tunapambana kuzuia maambukizi haya ili kuokoa maisha ya watu wetu na nguvu kazi kwa Taifa letu pia," Amesema Lulu.


 Waziri Mkuu Kassim Majaliwa (katikati) akiwa na viongozi wa Asasi zisizo za kiserikali (AZAKI) ambao walifika ofisini kwake kutoa msaada wa kusaidia mapambano dhidi ya maambukizi ya ugonjwa wa Corona.  Wa pili kutoka kulia ni Rais wa Foundation for Civil Society, Dk Stigimata Tenga, anaefuta ni Mkurugenzi wa LSF, Lulu Ngwanakilala na kulia kushoto ni Mkurugenzi wa Chama cha Wanasheria Wanawake (TAWLA), Time Mwambipile.
 Mkurugenzi kutoka Shirika la LSF, Lulu Ngwanakilala akizungumza na wandishi wa habari jijini Dodoma leo baada ya yeye na wadau wengine wa Asasi zisizo za kiserikali AZAKI kuahidi kuchangia Sh Milioni 79 kusaidia mapambano dhidi ya ugonjwa wa Corona.
 Rais wa Foundation for Civil Society, Dk Stigimata Tenga akizungumza na wandishi wa habari jijini Dodoma baada ya kuchangia Sh Milioni 79 kwa kamati ya kupambana na ugonjwa wa Corona inayoongozwa na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa leo jijini Dodoma.

 Viongozi wa Asasi zisizo za kiserikali AZAKI 2 wakizungumza na Wandishi wa habari mbalimbali jijini Dodoma baada ya kutoa kuchangia Sh Milioni 79 kwa kamati ya kupambana na ugonjwa wa Corona inayoongozwa na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...