Mkuu
wa Wilaya ya Dodoma, Patrobas Katambi akizungumza wakati wa hafla ya
kupokea vifaa vya kupambana na maambukizi ya ugonjwa wa Corona
vilivyotolewa na Kanisa la Anglikana Dayosisi ya Dodoma
Baadhi
ya vifaa ya kuzuia maambukizi ya ugonjwa wa Corona vilivyotolewa leo na
Kanisa la Anglikana Dayosisi ya Dodoma kwa Mkuu wa Wilaya ya Dodoma
leo.
Askofu
wa Kanisa la Anglikana Dayosisi ya Dodoma, Dk Dickson Chilongani
akizungumza wakati wa hafla ya kugawa vifaa vya kupambana na ugonjwa wa
Corona.
Charles James, Michuzi TV
MKUU wa Wilaya ya Dodoma, Patrobas Katambi amepokea vifaa vya kupambana na maambukizi ya ugonjwa wa Corona vyenye thamani ya Sh Milioni 16.5.
Vifaa hivyo vimetolewa na Kanisa la Anglikana Dayosisi ya Dodoma ambapo Askofu wake Dk Dickson Chilongani alikabidhi vifaa ikiwa ni jitihada za kuunga mkono serikali katika mapambano ya ugonjwa huo.
Akizungumza katika hafla ya makabidhiano hayo, DC Katambi amelishukuru kanisa hilo kwa mchango wao huo ambao amesema una thamani kubwa kwa serikali na wananchi wote wa Dodoma.
" Tunawashukuru sana viongozi wetu wa Kanisa kwa namna ambavyo mmeungana na serikali katika mapambano ya ugonjwa huu, tunawaahidi kwamba vifaa hivi vitawafikia wananchi wote waliokusudiwa hasa kwenye maeneo yenye mikusanyiko.
Niwaombe wananchi waendelee kufuata masharti yanayotolewa na wataalamu wetu wa afya na viongozi wakuu, tutumie vitakasa mikono lakini pia tuepuke mikusanyiko isiyo na ulazima," Amesema DC Katambi.
Amesema tangu kuingia kwa ugonjwa huu Rais Dk John Magufuli amechukua hatua nyingi muhimu zenye lengo la kuwaepusha wananchi wake na maambukizi ya Corona.
" Hakika Rais Magufuli ni wa mfano amevunja mbio za Mwenge, amevunja sherehe za Muungano na Sikukuu ya Wafanyakazi lengo likiwa kuepusha mikusanyiko lakini pia fedha zilizokua zimetengwa kwenye shughuli hizo amezipeleka kwenye mapambano ya Corona. Huyu ni Rais wa mfano sana," Amesema Katambi.
Kwa upande wake Askofu wa Dayosisi hiyo, Dk Chilongani amesema kitendo cha Rais Magufuli kuruhusu watu kuendelea kuabudu kwenye nyumba za ibada ni ishara kwamba yeye ni kiongozi hasa aliyeletwa na Mungu.
" Tunashuhudia Nchi za wenzetu wamepiga marufuku hata watu kuabudu makanisani na misikitini, lakini Sisi Rais wetu ameruhusu. Huyu ni kiongozi wa kuigwa na tunaamini tutaushinda ugonjwa huu kwa Uwezo wa Mungu," Amesema Dk Chilongani.
Amesema Dayosisi ya Dodoma imekua ikihudumia Wilaya tatu za Dodoma, Bahi na Chamwino na kwamba vifaa hivyo vitagaiwa sawasawa kwa kila Wilaya.
" Vifaa tulivyotoa ni ndoo, vitakasa mikono, vifunga mikono, mdomo, pua pamoja na pampu za kupulizia dawa. Vyote hivi tunagawa kwa wilaya zote tatu na jumla ya thamani yake ni Milioni 49.5 ambapo kila Wilaya itagharimu Sh Milioni 16.5," Amesema Dk Chilongani.

Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...