Charles James, Globu ya Jamii

SPIKA wa Bunge, Job Ndugai amekataa kusomwa kwa hotuba ya Kiongozi wa Kambi Rasmi ya Upinzani bungeni kuhusu hotuba ya Waziri Mkuu kwa kile alichoeleza kuwa zina shida ikiwemo kuwa na mambo mengi ya kubuni.

Amesema aliipata hotuba hiyo mapema na kuipitia ambapo amebaini kuwa na mambo mengi ya kubahatisha huku ikiwa haijazingatia kanuni za kiuandishi.

Amesema hawezi kuruhusu mambo ya mwaka wa kwanza na wa pili wa Bunge kufanywa katika mwaka wa tano na hivyo kusema ni lazima waende na viwango.

" Hii hotuba nimeipitia ina shida nyingi sana za herufi na makosa ya kiuchapaji ukiitoa hii kwenye mitandao inaenda duniani, ni sentensi tu zinapigwa kama tuko kwenye mkutano kule Kongwa sasa inatoa picha ya kwamba hawa watu hawako makini.

Lakini pia kuna lugha zenye shida, inaisema vibaya muhimili wa Mahakama kwa kuanzia baadhi ya maamuzi ya Mahakama na ikiwepo baadhi ya mambo ambayo yapo huko mahakamani kama suala la Wakurugenzi kusimamia au kutosimamia uchaguzi limejaa humu, masuala ya CAG aliepita pia yamo humu," Amesema Ndugai.

Amesema hotuba hiyo pia ina matumizi mabaya ya jina la Rais na mwenendo wa Rais jambo ambalo kanuni zinakataza hasa kanuni ile ya 64 pamoja na kulihukumu Bunge la 11.

" Ndio maana na wengine walioendelea na kiburi hiko mnaona hata huko mtaani matokeo yake ni hayo hayo tu ya mipambano isiyokua na sababu.

Sisi ni wabunge na mimi ni mbunge lakini inabidi tutambue kuna maeneo ni stricted areas na mojawapo ya maeneo hayo ni yale ya majeshi mbalimbali sasa mbunge ukienda kwenye maeneo hayo na ukaambiwa utoke halafu usitoke likakupata la kukupata sijui Spika akuteteaje kwenye maeneo kama hayo," Amesema Ndugai.

Amesema kwa ujumla wake hotuba za upinzani wangekua wanaandika kwa umoja wao zisingefika zilipofika kwani kama ni hotuba ya Waziri Mkuu wangeandika katika muktadha huo wa hotuba hiyo.

Spika Ndugai amesema kwa mwendo wanaoenda wapinzani hotuba zao zitakua hazisomwi kwani safari haitokua anawasahihisha pale wanapokiuka kanuni.

" Tuhuma zisizo na sababu ooh Tundu Lisu hajalipwa mishahara  yake na posho, Tundu hadai hata shilingi moja hata mshahara, vitu vya kuzusha kila siku tuwe tunabishana mambo ambayo hayana mbele wala nyuma ni lazima tuende vizuri," Amesema Spika Ndugai.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...