Benki ya Exim sambamba na wafanyakazi wa benki hiyo hii leo wamekabidhi msaada ya vyakula kwenye vituo vinne vya kulelea yatima na watoto wanaoishi kwenye mazingira magumu vilivyopo katika mikoa ya Dar es Salaam, Zanzibar, Mtwara na Tanga.

Ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa Mpango wa Uwajibikaji kwa Jamii (CSR) unaotekelezwa na benki hiyo unaofahamika kwa jina "Exim Cares", msaada huo ulilenga kuwawezesha watoto hao waweze kufurahia Sikukuu ya Eid-Ul-Fitr.

Kwa upande wa jiji la Dar es Salaam zoezi hilo liliongozwa na Mkuu wa Idara Masoko na Mawasiliano wa benki hiyo Bw Stanley Kafu ambapo akiwa kwenye kituo cha kulelea watoto yatima cha Malaika Kids, kilichopo wilayani Kinondoni, alitumia fursa hiyo kuwasisitiza watoto wanaoishi kwenye vituo hivyo kusoma kwa bidii kwa kuwa taifa linategemea mchango wao katika kufanikisha maendeleo.

Msaada huo ulihusisha vyakula vya aina mbalimbali ikiwemo mchele, mafuta ya kupikia, sukari, maharage pamoja na vinywaji .

“Zikiwa zimesalia siku chache tu kabla ya kusherehekea Sikukuu ya Eid Ul Fitr, Benki ya Exim tuliona ni vema tusherehekee pamoja na watoto yatima pamoja na wale wanaoishi kwenye mazingira magumu kwa kuwapatia mahitaji haya muhimu ili na wao waweze kufurahia siku hiyo muhimu kama wenzao waliopo majumbani…tunashukuru wametupokea vizuri na wameonyesha kufurahishwa na hilo.’’ Alisema

Akizungumza mara baada ya kupokea msaada huo, Mlezi wa kituo hicho Bi Neema Mohamed aliishukuru benki hiyo kwa wema huo huku akitoa wito kwa taasisi nyingine pamoja na watu binafsi kujitokeza pia ili kusaidia watoto wanaoishi kwenye vituo hivyo kwa kuwa mahitaji bado ni makubwa.

Baadhi ya wafanyakazi wa Benki ya Exim Tanzania wakiongozwa na Mkuu wa Idara Masoko na Mawasiliano wa benki hiyo Bw Stanley Kafu (Kushoto) wakikabidhi msaada ya vyakula kwa walezi wa kituo cha kulelea watoto yatima cha Malaika Kids kilichopo Wilayani Kinondoni jijini Dar es Salaam ili kuwawezesha watoto hao waweze kufurahia Sikukuu ya Eid-Ul-Fitr kama watoto wengine waliopo majumbani. Msaada wa aina hiyo pia ulitolewa na benki hiyo kwenye mikoa ya Mtwara, Tanga na Zanzibar.
Baadhi ya wafanyakazi wa Benki ya Exim Tanzania wakishusha msaada ya vyakula kwa walezi wa kituo cha kulelea watoto yatima cha Malaika Kids kilichopo Wilayani Kinondoni jijini Dar es Salaam ili kuwawezesha watoto hao waweze kufurahia Sikukuu ya Eid-Ul-Fitr kama watoto wengine waliopo majumbani. Msaada wa aina hiyo pia ulitolewa na benki hiyo kwenye mikoa ya Mtwara, Tanga na Zanzibar.
Meneja wa kituo cha kulelea watoto yatima cha Malaika Kids kilichopo Wilayani Kinondoni jijini Dar es Salaam Bw Charles Nyimbo akielezea wasifu wa kituo hicho kwa wafanyakazi wa Benki ya Exim wakati wa tukio hilo.


Meneja Mwandamizi wa benki ya Exim Zanzibar Bw Mwinyimkuu Ngalima ( wa tatu kushoto) sambamba na Mkuu wa Mkoa Mjini Magharibi Ali Hassani (katikati) wakikabidhi msaada ya vyakula kwa walezi na watoto wa kituo cha kulelea watoto yatima cha Muzdalifah Charitable Organization kilichopo mjini humo ili kuwawezesha watoto hao waweze kufurahia Sikukuu ya Eid-Ul-Fitr kama watoto wengine waliopo majumbani. Msaada wa aina hiyo pia ulitolewa na benki hiyo kwenye mikoa ya Mtwara, Tanga na Dar es Salaam.

Sehemu ya msaada wa chakula uliotolewa na benki ya Exim Zanzibar kwa ajili ya kituo cha kulelea watoto yatima cha Muzdalifah Charitable Organization kilichopo mjini humo.

Meneja wa benki ya Exim jijini Tanga Bw Ibrahimu Ukwaju (Kulia) akikabidhi msaada ya vyakula kwa walezi na watoto wa kituo cha kulelea watoto yatima cha Goodwill Orphanage kilichopo jijini humo ili kuwawezesha watoto hao waweze kufurahia Sikukuu ya Eid-Ul-Fitr kama watoto wengine waliopo majumbani. Msaada wa aina hiyo pia ulitolewa na benki hiyo kwenye mikoa ya Mtwara, Zanzibar na Dar es Salaam.

Baadhi ya wafanyakazi wa benki ya Exim jijini Tanga wakiwa kwenye picha ya pamoja na walezi pamoja na watoto wa kituo cha kulelea watoto yatima cha Goodwill Orphanage kilichopo jijini humo baada ya kukabidhi msaada huo.

Meneja wa benki ya Exim Mkoani Mtwara Bw John Kayombo (kushoto) akikabidhi msaada ya vyakula kwa watoto wa kituo cha kulelea watoto yatima cha EAGT Rahaleo Orphanage Centre kilichopo mkoani humo ili kuwawezesha watoto hao waweze kufurahia Sikukuu ya Eid-Ul-Fitr kama watoto wengine waliopo majumbani. Msaada wa aina hiyo pia ulitolewa na benki hiyo kwenye mikoa ya Tanga, Zanzibar na Dar es Salaam.

Meneja Msaidizi wa benki ya Exim Mkoani Mtwara Bw John Kayombo (alieketi) pamoja na wafanyakazi wengine wa benki hiyo wakiwa kwenye picha ya pamoja na walezi pamoja na watoto wa kituo cha kulelea watoto yatima cha EAGT Rahaleo Orphanage Centre kilichopo mkoani humo baada ya kukabidhi msaada wa vyakula kwa watoto hao.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...