Na COSTECH

Takwimu kutoka kampuni in inayojihusisha na mikopo ya Nyumba Tanzania (TMRC) zinaonyesha kuwa Tanzania ina upungufu wa nyumba milioni tatu. Takwimu hizo pia zinaonyesha  kuwa nchini Tanzania kila mwaka kuna ongezeko la mahitaji ya nyumba 200,000. Sababukubwa za ongezeko la mahitaji ya nyumba nchini ni pamoja na gharama kubwa ya vifaa vya ujenzi.
Gharama kubwa ya vifaa vya ujenzi inasababisha wananchi wengi kuishi kwenye nyumba zisizo bora kwani hujenga nyumba zao kwa kutumia vifaa duni kwa lengo la kujipatia sehemu ya kujisitiri. Hii huhatarisha afya na maisha yao kwa ujumla.
Ili kutatua changamoto ya gharama za vifaa vya ujenzi, Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH) imemuibua na kumuwezesha Mbunifu Mwalimu Said Abeid aliye buni utengenezaji wa matofali na malumalu  kwa kutumia taka ngumu.
 “Nachanganya madini ya ulanga na pumba za mpunga kutengeneza matofali na malumalu. Matofali ninayo tengeneza huwa mepesi, na yanadumu kwa muda mrefu,” anasema Mwalimu Said.
Haikuwa kazi rahisi kuupata ubunifu huo. Alipopata wazo la kutengeneza matofali hayo alijiuliza kama malighafi zinapatikana nchini hivyo akalazimika kwenda kwa Wakala wa Utafiti wa Madini Tanzania (GST) walikomthibitishia kuwa yapo ya kutosha.
Baada ya hapo akaingia maabara kuanza kujaribisha kanuni (formula) mbalimbali kabla hajapata alichokuwa anakitafuta; yaani, tofali jepesi litakalodumu kwa muda mrefu.
“Kwenye mataifa yaliyoendelea, mfano Ulaya na Amerika wameachana na matumizi ya matofali ya mchanga (blocks). Wanatumia matofali haya ambayo ni mepesi na yanadumu kwa muda mrefu. Yanafaa sana kujengea nyumba za ghorofa,” anasema mwalimu huyo.
Licha ya wepesi wa matofauti hayo, ipo faida nyingine muhimu kwa afya ya binadamu. Mwalimu anasema, matofali yaliyo zoeleka yatokanayo na udongo wa kawaida, hupitisha joto hivyo kuifanya nyumba iwe na joto linalobadilika kulingana na hali ya hewa.
Yaani hali ya hewa ikiwa ya joto basi ndani ya nyumba huwa na joto pia na hali ya hewa ikiwa ya baridi basi ndani huwa baridi pia. Matofali na malumalu alivyobuni Mwalimu Said hayaathiriwi na hali ya hewa.
“Ukijenga kwa matofali haya na ukatumia malumalu ninazo tengeneza, hautakuwa na haja ya kuweka zuria sakafuni kukwepa baridi wala kutumia kiyoyozi au feni kwa ajili ya ongezeko la joto kwani ongezeko la joto nje halitoingia ndani. Matofali na malumalu ninazotengeneza hazipitishi joto kirahisi hivyo mabadiliko ya joto nje hautoyahisi ndani ya nyumba yako,” anasema Mwalimu Said. Said ni mwalimu anafundisha somo la fizikia Chuo cha Madini Dodoma.
Ubunifu wa kutengeneza matoifali na malumalu kwa kutumia taka ngumu ulimfanya Mwalimu Said awe miongoni mwa zaidi ya wabunifu 50 walioibuka washindi wa Mashindano ya Kitaifa ya Sayansi, Tekonolojia na Ubunifu (MAKISATU) yanayoratibiwa kila mwaka na Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH) kwa ajili ya kuwaibua wabunifu na kuishauri Serikali namna ya kuwaendeleza wabunifu hao.
COSTECH ilimpa Mwalimu Said kiasi cha Shilingi za kitanzania milioni 47 kwa ajili ya kununua mitambo ya uzalishaji wa matofali na malumalu zinazo tengenezwa kwa kutumia taka ngumu kwa lengo la kusaidia jamii inayomzunguka na watanzania kwa ujumla.
“Naishukuru sana COSTECH kwa ruzuku hii, kwani bila ufadhili wa Tume hii ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia  wazo na ubunifu huu ungeishia kwenye vitabu tu bila kuwanufaisha Watanzania. Tayari chuo kimenipa eneo kwa ajili ya uzalishaji wa awali,” anasema Mwalimu Saed.

Mwalimu Said anatumia mfumo wa fedha wa Chuo, na uongozi wa chuo unamsaidia kuendesha na kupangilia utafiti na shughuli zake za ubunifu ili kuhakikisha matokeo chanya ya ubunifu wake yanainufaisha jamii.
Kaimu mkuu wa Chuo cha Madini Dodoma, Ivanus Kapila anasema chuo cha madini Dodoma kinamsimamia Said kuhakikisha ubunifu wake unakuwa naviwango bora wenye kukidhi viwango vya  kitaifa na kimataifa.
“Chuo kinamruhusu kutumia maabara kwa ajili ya utafiti wake bila malipo yoyote. Tunafurahi kwa ubunifu wake kwani tunaamini utahamasisha uanzishaji wa viwanda vidogo. Vilevile Mwalimu Said ameomba awafundishe wanafunzi waliopo kuhusu mradi wake ili waweze kujiajiri pindi watakapohitimu masomo yao,” anasema Kaimu mkuu wa Chuo cha Madini ndgugu Ivanus Kapila.
Kwa mwanga aliouonyesha Said, makamu mkuu wa Chuo cha Madini Dodoma amesema  itahamasisha  wabunifu kuongezeka chuoni hapo na hivi sasa kuna wataalamu wanafanya utafiti wa kutengeneza mtambo utakaochenjua dhahabu bila kutumia zebaki. “Said ameonesha njia kwa kutumia malighafi ambazo hazikuonekana kuwa na tija kwenye sekta ya ujenzi. Hii ni fursa ya kukuza uchumi,” anasema Kapila.
Mbunifu Mwalimu Said Abeid akizungmza na waandishi wa habari.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...