Na Leandra Gabriel, Michuzi TV
LEO MEI 12 dunia inasherehekea siku ya Wauguzi na wakunga duniani huku umuhimu na mchango mkubwa wao katika sekta ya afya ukigusa mamilioni ya wananchi hasa wanawake.
Muasisi wa siku hii adhimu kwa wauguzi na wakunga ni Florence Nightingale; "Mwanamke wa Taa" ambaye alisimama kidete katika kuinua viwango vya uuguzi pamoja kuwaelimisha Wauguzi.
Harakati zake zilianza baada ya kufika nchini Uturuki mwaka 1854 ambapo nchi hiyo ilikuwa katika vita ya Krimea, Florence alikuta hali za hospitali ni mbaya,askari waliojeruhiwa walikuwa wamelazwa katika uchafu huku wengi wakifariki kwa magonjwa ya kuambukizwa na si vidonda vyao, hali hiyo ilimfanya yeye na wasaidizi wake 38 kukagua na kufanya usafi hospitalini hapo.
Kabla ya Nightingale taaluma ya uuguzi haikuthaminiwa ilionekana ni taaluma ya chini, Florence aliipigania na kuinua viwango vya uuguzi akiangazia hali ya usafi, kuelimisha wagonjwa ili waweze kujitunza wenyewe na kuangalia hali za wagonjwa kwa ukaribu zaidi na alipokuwa akienda kuwatizama wagonjwa nyakati za usiku alibeba taa na akaitwa "Mwanamke wa Taa"
Florence Nightingale maarufu kama 'Mwanamke wa Taa" alizaliwa Mei 12, 1820 nchini Italy na kufariki Agosti 3, 1860 London, Uingereza alizaliwa katika familia ya kitajiri ambayo ilipinga vikali binti yao kujiunga na fani hiyo lakini ilishindikana Florence akajitoa katika kuwahudumia wagonjwa na kueleza huo ni wito uliotoka kwa Mungu.
Florence alienda nchini Ujerumani ambako alijifunza fani ya uuguzi katika taasisi ya kilutheri na aliporejea Uingereza alipewa uongozi katika zahanati ya wanawake.
Licha ya kujitoa na kuwahudumia wagonjwa Florence alianzisha vyuo vya uuguzi na hospitali ikiwemo chuo cha uuguzi kilichofunguliwa mwaka 1860 kiitwacho Nightingale School of Nursing kilichopo katika hospitali ya St. Thomas, nchini Uingereza pia aliandika vitabu mbalimbali vya uuguzi na ukunga.
Siku hii ya Wauguzi inakumbukwa Mei 12 kila mwaka ambayo ni siku ya kuzaliwa Muasisi huyo huku kumbukizi hiyo ikilenga kukumbuka mchango wake kwa wauguzi na sekta ya afya kwa ujumla.

Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...