Na Issa Michuzi
"Mbuyu umeondoka. Kisiki kimeng'oka.
Moja ya alama kubwa za Sanaa nchini imetoweka…."
Hayo ni maneno ya Rais wa Shirikisho la Sanaa za Ufundi Tanzania Mkushi Adrian Nyangamale wakati akimuelezea Robino Ntila, msanii nguli mpenda maendeleo ya Sanaa.
Robino, aliyezaliwa Ndanda, Masasi, mkoani Mtwara mwaka 1953, na aliewahi kuwa kiongozi mahiri wa mwanzo wa Nyumba ya Sanaa jijini Dar es salaam kabla haijafa na Mjumbe wa Bodi ya Baraza la Sanaa la Tanzania (BASATA), amefariki dunia Alhamisi Mei 21, 2020 katika hospitali ya Temeke jijini Dar es salaam alikokuwa akipatiwa matibabu.
“Marehemu Ntila pia alikuwa mmoja wa wanzilishi wa Chama Cha Wasanii Wachoraji Tanzania (Fine Artists' Association of Tanzania), mshauri mzuri wa Sanaa aliyependa kujichang'anya na vijana. Ni msiba mkubwa na pigo kubwa kwa sekta ya Sanaa nchini.
“Nimepokea kwa mstuko na masikitiko makubwa kifo cha Mzee Robino Ntila a.k.a Lufombo, Mungu amrehemu na apumnzishe mahali pema peponi Amina”, anasema Nyangamalle katika salamu zake katika grupu la Whatsapp la Jamvi la TAFCA.
Msanii George Danford Nahamiani Mrope anasema: “Binafsi nilimfahamu Robino tangu miaka hiyo ya Tanzania Artist Association… namkumbuka siku aliyonikabidhi sh 15,000/ zawadi yangu pale Nyumba ya Sanaa mwaka 1995 baada ya kuwa mshindi wa pili wa shindano la picha, theme ilikuwa “ Uzazi wa Mpango lililofadhiliwa na GTZ.
“Namkumbuka pia kuwa nae kwenye workshop ya hitching technique 1996 kama sikosei University of UDSM iliyofadhiliwa na Shirika la Sweden, na kukutana nae kwenye hafla mbali mbali. Msanii huyu Nguli alikuwa hakosekani katika kila shughuli ya kisanii. Zaidi ya yote hakika kama President ulivyomkumbuka Robinio alikuwa mwenyewe sifa ya upekee wa kujichanganya na vijana!!! Umefurahisha sanaaa” ana sema Mrope aliyepata kuwa mwalimu wa Sanaa shule ya Sekondari ya Minaki.
Mrope na Wasanii wengine wameendelea kutoa pole kwa Jamii nzima ya wabunifu nchini kwa msiba mkubwa walioupata, wakieleza kwamba Mzee Ntilla, pamoja na hizi sifa alizokuwa nazo, pia alitoa mchango mkubwa kwa watafiti wa masuala ya Sanaa hapa nchini. Mungu ampumzishe Mahala Pema.
Licha ya kuwa mratibu wa mashindano ya Sanaa, Mzee Robino ndiye aliyetoa wazo la kuanzisha chama cha Fine Artists' Association of Tanzania, ambapo siku alipotoa wazo hilo nguli kadhaa wa sanaa nchini walikuwepo na kuunga mkono hoja yake. Wasanii waliokuwepo kuwepo siku hiyo ni pamoja na Prof. Elias Jengo, Njoka, Mwl. Massanja, Mzee Hinju, Edward Pwuza, Tenga, Mnoni, James Gayo na wengine wengi. Philimon Mwassanga akachakuwa kuwa Mwenyekiti na Mzee Robino Ntila akawa Katibu. Hakika Mzee huyu ana mchango mkubwa sana katika tasnia na sekta nzima ya Sanaa.
Uongozi wa kituo cha Sanaa cha Nafasi Art umesema: "Siku ya leo, Mei 21, 2020, msanii mkubwa na rafiki yetu Robino Ntila ametutoka. Tutamkumbuka kwa mchango wake mwingi na mkubwa kwenye tasnia ya sanaa ya uoni Tanzania.
"Tungependa tuungane pamoja kama marafiki zake na jamaa katika kumkumbuka kwa kurekodi video fupi ukimuelezea Robino na kazi zake na tutumie tuzishirikishe kwenye kurasa zetu kama njia ya heshima ya kumbukumbu kwake. Asante na Apumzike mahali pepa peponi.
"Waweza kututumia kupitia whatsapp +255653757877 au Tu-tag katika kurasa zetu: @nafasiartspace".
Msanii mwingine anasema yote kwa yote mzee huyu katika utu uzima wake bado alikuwa mstari wa mbele kuipigania sanaa ya ufundi Tanzania bila kujali changamoto nyingi zilizopo kwenye tasnia hii. Nakumbuka mpaka wakati huu anatutoka kule Kenya kuna Maonesho ya wasanii kutokea Tanzania ambayo yali ingiliana na changamoto ya corona mpaka leo hii kazi zetu ziko kule Nairobi yeye akiwa msimamizi mkuu wa Maonesho hayo.Tuta mkumbuka kwa mengi. Apumzike kwa amani mzee wetu mpendwa Robino a.k.a Baba...
Mkongwe Deo Kafwa anasema: “Sifa nyingi zimetolewa kuhusu Marehemu Robino. Itoshe tu kusema Asante Mungu kwa zawadi ya mtu huyu kwetu sisi tuliyefanya naye kazi Nyumba ya Sanaa. Naelezwa kuwa mazishi yake yatafanyika Jumamosi Msiba upo nyumbani kwake Mbagala Kimbangulile.Bwana alitoa bwana ametwaa jina la bwana lihimidiwe.
Mwa
ndishi wa makala haya, ambaye pia ni mmoja wa watu waliokuwa wa karibu wa marehemu Robino, anasema kwa uchungu kwamba baada ya hayati Jah Kimbute, MKUSHI mwengine katangulia mbele ya haki. Anakumbuka sana vikao vyao kwenye kahawa Nyumba ya Sanaa na YMCA kila jioni. Kwa kweli inauma mno.
"Robino na Jah Kimbute ndio waliotoa jina hilo la MKUSHI kwa sie marafiki wa sanaa tuliokuwa pamoja kwa zaidi ya miaka 20 pale Nyumba ya Sanaa na YMCA. Hadi leo tunaitana hivyo na tutaendelea kuitana hivyo kuwaenzi Robino na Kimbute", anasema.
Kwa mujibu wa Chris Ntila, mazishi ya Robino yatakua jumamosi makaburi ya SAKU Mbagala njia ya kwenda Chamazi. Mwili utafika nyumbani kwa marehemu Mbagala Kimbangulile saa 4 kwa ajili ya kuaga ambapo saa 5 itakuwa ibada kanisani na saa 7 makaburini.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...