NA BALTAZAR MASHAKA, MWANZA

MWANAFUNZI wa darasa la tano katika Shule ya Msingi Katoba ya wilayani Muleba, Aristidia John, amepata msaada wa baiskeli ya magurudumu matatu (Wheerchair).

Baiskeli hiyo iliyotolewa na taasisi ya The Desk & Chair Foundation ili kumrahisishia usafiri ilikabidhiwa jana kwa mtoto huyo na Mwenyekiti wa Klabu ya Waandishi wa Habari Mkoa wa Mwanza (MPC) .

Aristidia ambaye ni mwanafunzi wa darasa la tano katika Shule ya Msingi Katoba wilayani Muleba, alifanyiwa upasuaji na kuondolewa mguu wa kulia katika Hospitali ya Rufaa ya Kanda ya Bugando baada ya kushambuliwa na saratani.

Akizungumza baada ya kukabidhiwa baiskeli hiyo, mtoto huyo aliwashukuru waandishi wa habari wa vyombo mbalimbali waliowezesha kupatikana fedha za kugharamia matibabu yake.

Alisema baada ya kupata maradhi hayo alikata tamaa ya kutimiza ndoto zake za maisha na masomo kabla ya The Desk & Chair Foudation kujitolea kugharamia matibabu yake na huduma nyingine za kibinadamu na kuhakikisha afy yake inaimarika.

“Nawashukuru sana waandishi wa habari kupitia kalamu zenu kilio changu kilisikika kwa Watanzania ambpo baadhi waliguswa na tatizo la ugonjwa wangu.Namshukuru Mwenyekiti wa The Desk & Chair Sibtain Meghjee kwa moyo wake wa kujitoa,sikuwa na matumaini tena ya kupona bila yeye hivyo Mungu amjalie afya njema,” alisema Aristidia bila kuwasahau madaktari na wauguzi wa Hospitali ya Bugando na familia ya watumishi wa mgodi wa GGM.

Alieleza kuwa ndoto yake ni kuwa mwalimu wa kuwafundisha watoto na kuwapa maarifa yatakayowasaidia maishani mwao, hivyo akirejea shuleni atajifunza kwa bidii ili atimize malengo yake na kwamba hali yake inaimarika .

Alieleza zaidi baada ya kufanyiwa upasuaji anaamini Mungu atamjalia na kupona na kurejea shuleni kuendelea na masomo ili kutizima ndoto yake lakini anakabiliwa na umaskini wa kipato wa familia unaoweza kuwa kikwazo.

Alitumia fursa hiyo kuwaomba Watanzania wenye uwezo wamsaidie kupata shule ya gharama nafuu aweze kusoma akiwa katika mazingira ya shule badala ya kutoka umbali mrefu kama ilivyokuwa awali kabla ya kupata ulemavu huo wa kudumu.

“Kutokana na hali niliyo nayo na uchumi duni wa familia, niwaombe Watanzania wanisaidie kupata shule ya gharama nafuu za masomo, kwa sasa itakuwa vigumu kutembea umbali mrefu kwenda shule kwa kutumia magongo ikizingatiwa familia yangu inaishi maisha duni na mimi nataka niwe mwalimu baada ya kuhitimu,”alisema Aristidia.

Mama wa mtoto huyo Agnes Bosco hakuwa na zaidi ya kusema mbali na kumshukuru Mungu, wafadhili na waandishi wa habari kwa kuwezesha matibabu ya mwanaye.

“Mungu awabariki sana na nawaombea sana mbarikiwe katika shughuli zenu pamoja na wafadhili wakiwemo madaktari wa Bugando,”alisema.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa MPC Edwin Soko, alisema klabu hiyo itaendelea kutafuta wafadhili watakaomsaidia Aristidia mguu saidizi (bandia) lakini pia watu watakaoweza kulimpia gharama za masomo kwenye shule zinazofundisha kwa lugha ya kimataifa.
 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...