Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akimkabidhi Hati ya
Makabidhiano ya zawadi ya Ndege aina ya Tausi 25 kwa Mama Maria Nyerere
mjane wa Baba wa Taifa Mwalimu Julius Nyerere kwa ajili ya kuwafuga
katika Makazi yake, hafla hiyo fupi ilifanyika katika viwanja vya Ikulu
ya Chamwino Mkoani Dodoma.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akimkabidhi hati ya
Makabidhiano ya ndege aina ya Tausi 25 kwa Rais Mstaafu wa Awamu ya Pili
Mzee Ali Hassan Mwinyi kwa ajili ya kuwafuga katika makazi yake. Hafla
ya Makabidhiano hayo imefanyika katika viwanja vya Ikulu ya Chamwino
mkoani Dodoma.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akimkabidhi hati ya
Makabidhiano ya ndege aina ya Tausi 25 kwa Rais Mstaafu wa awamu ya Tatu
Benjamin Mkapa kwa ajili ya kuwafuga katika makazi yake. Hafla ya
Makabidhiano hayo imefanyika katika viwanja vya Ikulu ya Chamwino mkoani
Dodoma.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akimkabidhi hati ya
Makabidhiano ya ndege aina ya Tausi 25 kwa Rais Mstaafu wa awamu ya nne
Jakaya Kikwete kwa ajili ya kuwafuga katika makazi yake. Hafla ya
Makabidhiano hayo imefanyika katika viwanja vya Ikulu ya Chamwino mkoani
Dodoma.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika picha ya
pamoja na Viongozi hao Wakuu wastaafu mara baada ya kuwakabidhi zawadi
ya ndege aina ya Tausi.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza katika hafla
hiyo fupi ya Makabidhiano ya zawadi ya ndege aina ya Tausi.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akimsikiliza Rais Mstaafu
wa Awamu ya nne Dkt. Jakaya Kikwete wakati akitoa neno la Shukrani kwa
niaba ya Marais wenzake wastaafu.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akifurahia jambo na Rais
Mstaafu wa Awamu ya Pili Mzee Ali Hassan Mwinyi pamoja na Rais Mstaafu
wa Awamu ya nne Dkt. Jakaya Kikwete mara baada ya hafla fupi ya
Makabidhiano ya ndege aina ya Tausi katika Ikulu ya Chamwino mkoani
Dodoma.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwasili katika viwanja
vya Ikulu ya Chamwino na Rais Mstaafu wa Awamu ya Pili Mzee Ali Hassan
Mwinyi, Mjane wa Baba wa Taifa Mama Maria Nyerere pamoja na Rais Mstaafu
wa awamu ya Tatu Benjamin Mkapa. PICHA NA IKULU
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...