NA MWAMVUA MWINYI,PWANI
USHIRIKA
wa Umwagiliaji Ruvu (CHAURU) unaofanya kilimo katika mashamba ya Ruvu
,Kata ya Vigwaza Bagamoyo, Pwani, Unahitaji sh .bilioni. 11 kwa ajili ya
kununua mashine ya kuondoa maji kwenye mashamba ya wanachama wake.
Hatua
hiyo inalenga kuondokana na changamoto ya mashamba kuingia maji, hasa
nyakati za mvua hali inayosababisha kushindwa kuendeleza kilimo.
Hayo
yalibainishwa na Mwenyekiti wa CHAURU Sadala Chacha, alipozungumza na
waandishi wa habari katika ofisi za mashamba hayo, ambapo alisema suala
hilo limepitishwa na wanachama, na tayari wameshapeleka maombi hayo
katika benki ya TIB.
"Hatua
hii inalenga kuboresha ufanisi kwa wanachama waweze kupata mafanikio
zaidi katika sekta ya kilimo ,tumepeleka ombi la pesa kiasi cha sh.
bilioni 11 tutazonunua mashine inayonyonya maji yanayotuama
mashambani,"; mwaka huu wa kilimo 2019/2020 mashamba yetu yamevamiwa na
maji, hivyo kusababisha baadhi yetu kushindwa kupanda," alisema Chacha.
Aidha
Chacha alieleza, CHAURU inakabiliwa na changamoto kubwa ya kutengeneza
miundombinu ya mifereji na baadhi ya matuta ya kuzuia maji yasiathiri
mashamba.
Nae meneja
wa ushirika huo ,Victoria Olotu alieleza pia kuna changamoto ya uwepo wa
mnyama Kiboko, anayeonekana kwenye mashamba hayo nyakati za jioni, hali
inayosababisha hofu kubwa kwa wana-Ushirika hao.
Alisema
kwamba kutokana na hali hiyo ameshatoa taarifa kwa viongozi wanaohusika
ili wafike kwa ajili ya kumswaga aweze kuondoka, hatimae wanachama
waweze kuendelea na shughuli zao kama kawaida.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...