NA YEREMIAS NGERANGERA…NAMTUMBO

Wananchi na wakulima wa mazao ya ufuta .soya ,choroko wilayani Namtumbo Mkoani Ruvuma wanaishukuru serikali kwa kuanzisha mfumo wa mauzo kwa njia ya stakabadhi ghalani ambao unawanufaisha wakulima.

Wakiongea kwenye mnada wa kwanza, wa pili na watatu katika ghala la ushirika lililopo katika mamlaka ya mji mdogo wa Namtumbo ulikokuwa unafanyika mnada huo ,wananchi na wakulima waliohudhuria mnada huo walisema serikali imelenga kuwanufaisha wakulima waliokuwa wanaonewa na madarali waliokuwa wanapata faida kubwa na kumkandamiza mkulima .

Shaban Kumbwani mkazi wa mamlaka ya mji mdogo wa Namtumbo na mkulima wa zao la ufuta alisema serikali imelenga kuwainua wananchi wake kwa madai kuwa amekuwa mkulima wa zao la ufuta muda mrefu akiuza kwa walanguzi (madalali) na hakuwahi kupata pesa nyingi kama anavyopata hivi sasa kwa kuuza kupitia mfumo wa stakabadhi ghalani.

Bwana Kubwani aliongeza kuwa madalali ndio waliokuwa wananufaika na nguvu za wakulima kwa kuchukua faida kubwa na mkulima kumwacha na fedha kidogo ambapo kwa sasa fedha zote zinaenda kwa mkulima na wakulima wanaona faida ya kilimo tofauti na huko nyuma alisema Kumbwani.

Pamoja na shukrani hizo bwana kumbwani anaiomba serikali kuingiza mazao yote yauzwe katika mfumo wa stakabadhi ghalani kwa kusisitiza hasa zao la mahindi na mpunga ambalo kwa mujibu wa yeye alidai bado yanawanyonya wakulima wa wilaya ya Namtumbo kwa kuendelea kuwaachia madalali wanunue mazao hayo.

“Wakulima tunaikubali dhamira njema ya serikali ya kuwainua wanyonge hasa wakulima ,tunaiomba serikali mazao yote yanunuliwe kwa mfumo wa stakabadhi ghalani kwani vyama vya ushirika AMCOS zimeonesha kusimamia vyema mauzo na wakulima wameanza kuonesha imani na vyama hivyo ,tunaiomba serikali waruhusu mazao yote yakusanywe na vyama vya ushirika ili wakulima wanufaike “ alisema Kumbwani.

Wilaya ya Namtumbo mkoani Ruvuma inafaa kwa kilimo cha mazao mbalimbali huku inajumla ya kilomita za mraba 20,735 na zaidi ya kilomita za mraba 11,000 zinafaa kwa kilimo na zinazotumika kwa kilimo kwa sasa ni kilomita za mraba 6000 pekee .

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...