Na Sixmund J. Begashe wa Makumbusho ya Taifa
Msanii
maarifu Nguza Mbangu Viking maarufu kama "Babu Seya" na Mkewe Desderie
P. Haule ambae pia ni Mkurugenzi wa Halmashauri ya Muheza Tanga,
wamefanya Utali wa ndani mjini Songea kwa kuitembelea Makumbusho ya Maji
Maji kwa lengo la kujifunza urithi wa historia ya Vita vya Maji Maji
vilivyo tokea miaka ya 1905 hadi 1907.
Akizungumza
baada ya kuitembelea Makumbusho hiyo Bw Viking ameipongeza Makumbusho
ya Taifa kwa kuhifadhi urithi huo wa kihistoria kwani umempatia nafasi
ya kujifunza kwa kuona namna mababu zetu walivyo tanguliza uzalendo
katika kupigania haki na heshma yetu.
"Nimejifunza
mambo mengi, japo yanaumiza sana lakini yanatupa faraja na ujarisiri
katika kuendelea kulinda heshma yetu kama watanzania, Mashujaa wa Maji
Maji wamesha timiza wajibu wao sasa kazi ni kwetu hasa katika kuunga
mkono jitihada za Mhe Rais wetu Dkt John Pombe Magufuli katika kuleta
maendeleo nchini" Alisema Bw Viking.
Nae
Mke wa Viking Bi Desderie Haule licha ya kufurahia Utalii huo wa ndani
katika kipindi chake cha likizo alisema kuwa ipo haja hasa vijana
kuitembelea Makumbusho hiyo ya Vita vya Maji Maji ili kujifunza,
uzalendo, upendo, kujituma na mengineyo ambavyo ni misingi bora ya
uongozi utakao nufaisha Taifa Leo kama tunavyo nufaika sasa kupitia Mhe
Rais wetu ambae ni Mzalendo Dkt John Pombe Magufuli
Mkurugenzi
Mkuu wa Makumbusho nchini Dkt Noel Lwoga ambae yupo Songea kikazi
amekutana watalii hao wa ndani (Familia ya Babu Seya) na kuwapongeza kwa
kuitembelea Makumbusho hiyo na kutoa wito kwa wakazi wa Ruvuma na wote
wanao ingia Songea kwenda katika Makumbusho hiyo ili kujione na
kujifunza historia hadhimu ya Taifa hili kupitia Vita vya Maji Maji.
Msanii Nguli nchini na Mkewe Bw Nguza Mbangu Viking (Babu Seya) wakipata
Maelezo kutoka kwa Mtaalamu wa Makumbusho ya Majimaji Songea Bw Erick
Soko juu ya Historia ya Vita vya Majimaji.
Kulia ni Mkurugenzi Mkuu wa Makumbusho ya Taifa Dkt Noel Lwoga
wakiwapongeza Bw Viking na Mke wake Bi Desderia Haule kwa kuitembelea
Makumbusho ya Majimaji Mjini Songea
Kulia Mkurugenzi Mkuu wa Makumbusho ya Taifa Dkt Noel Lwoga
akiongozana na Bw Viking na Mkewe wakitoka kuangalia Mnara wa Askari
uliopo Makumbusho ya Maji Maji Mjini Songea.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...