Na Said Mwishehe,Michuzi TV.

BAJETI imepita!Hiyo ndio habari ya Mjini kwa siku ya leo baada ya wabunge kupitisha kwa kishindo Bajeti ya Serikali kwa mwaka wa Fedha 2020/2021 yenye jumla ya Sh.trilioni 34.88.

Kura ambazo zimepigwa na wabunge na kufanikisha kuipitisha bejeti hiyo ni  kura za ndio 304 huku kura , 63 za hapana huku wabunge 18.Hata hivyo safari hii wabunge wa vyama vya upinzani wengi wao wamepiga kura ya ndio.

Kwa kukumbusha tu bajeti ya mwaka huu ndio ambayo imeungwa mkono zaidi kwa wabunge zaidi ya 300 kupitisha bajeti hiyo ikilinganishwa  na huko nyuma.

Katibu wa Bunge, Stephen Kigaigai, ameliambia Bunge leo Juni 15,2020 jijini Bungeni Mjini Dodoma kuwa idadi ya wabunge 371 ndio waliopiga kura na kati ya hao 304 walipiga kura ya ndio na wabunge 63 wakipiga kura ya hapana.

Baada ya matokeo hayo yaliyotangazwa na Katibu wa Bunge, ndipo aliposimama Spika wa Bunge Job Ndugai kutangaza kupitishwa kwa Bajeti Kuu ya Serikali.

Akizungumza mbele ya wabunge baada ya kupiga kura,Spika Ndugai alionesha kufurahishwa na idadi kubwa ya kura ya ndio huku akisikika akisema kuwa"Yajayo yanafurahisa, bajeti imeungwa mkono na idadi kubwa ya wabunge ambayo haijawahi kutokea."

Pamoja na mambo mengine Ndugai ametumia nafasi hiyo kumpongeza Waziri wa Fedha na Mipango Dk.Philip Mpango, Naibu Waziri wa Wizara ya Fedha Dk.Ashantu kijaji pamoja na watalaam wa kada mbalimbali wa wzara hiyo kwa kufanikisha kupitishwa kwa bajeti hiyo ya serikali."Hii ni bajeti ya mwisho kabla ya kuelekea kwenye Uchaguzi Mkuu wa Urais, Wabunge na Madiwani ambao utafanyika Oktoba 25 mwaka huu".
Waziri wa Fedha na Mipango Dk.Philip Mpango

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...