Na Said Mwishehe, Michuzi TV.

MBUNGE wa Jimbo la Iringa Mjini, Mchungaji Peter Msigwa(CHADEMA),ameshauri Bunge kutunga sheria ambazo hazitakuwa mzigo kwa Watanzania.

Mchungaji Msigwa amesema hayo leo Juni 10,2020 Bungeni Mjini Dodoma wakati anachangania Muswada wa Marekebisho ya Sheria mbalimbali ambao umewasilisha Bungeni.

"Moja ya jukumu la msingi la Bunge ni pamoja na kusimamia utungwaji wa sheria,hivyo wabunge wanaowao wajibu wa kusimamia utungwaji wa sheria ambazo hazitakuwa za ukandamizaji,"amesema Mchugaji Msigwa.

Amongeza hivyo ni makosa kuwa na sheria au mabadiliko ya sheria katika nchi bila wananchi kujua."Hivyo ni vema tuwe na sheria rafiki kwa wananchi."

Amesema sheria hazina macho na wala haziangalii aliyeko sasa peke yake, hivyo kuna umuhimu mkubwa wa kuhakikisheria kabla ya kutungwa inakuwa imekamilika na iko sawa sawa.

"Kuna kila sababu ya kuangalia kwa undani zaidi sheria ambazo zinatungwa na Bunge ili kuwa na tija kwa Watanzania wote kwani lengo la kuwa na sheria sio kutesa wananchi,"amesema Mchungaji Msigwa.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...