Na.Vero Ignatus.


Mkuu wa Wilaya ya Kiteto Mkoani Manyara Bwana Tumaini Magesa amewataka wafugaji na wakulima katika vijiji vitatu vya Kimbo;Allole na Napalai; vinavyounda ushirika wao wa kutunza ardhi kwa ajili ya malisho ya Mifugo unaofahamika kama OLENGAPA kuheshimu taratibu za hati miliki za kimila na usajili wa ushirika huo kwa faida ya kizazi cha sasa na kijacho.
Ametoa rai hiyo katika kijiji cha ENGANG’ONGARE alipokuwa akikabidhi hati miliki za kimila 9 ambapo hati hizo zimefadhiliwa kwa ufadhili wa Programu ya GSI-ICCA kupitia shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP).

Kwa upande wa Umoja wa Ulaya (EU) wakisaidia kupata Usajili wa Usharika wa wafugaji wa kongani tatu ambazo ni Kimbo, Allole na Napalai na kuendeleza nyanda za Malisho, uliopo katika mpango wa kimataifa wa kuendeleza maeneo yaliyohifadhiwa kwa kutumia taratibu za kiasili au kimila na kutekelezwa na Jumuiko la Mali Asili Tanzania (TNRF) na Muungano wa vijiji vya wafugaji kwa ajili ya kusaidiana (KINNAPA).

Bwana Magesa amesema ni vizuri kila eneo matumizi yake yawe yamepangwa na kujulikana kisheria; ili kuondoa changamoto ya migogoro ya ardhi, iliyokuwa ikijitokeza wilayani humo, miaka iliyopita; na pia kwa faida ya kizazi cha sasa na kijacho.

Baadhi ya wenyeviti wa vijiji hivyo pamoja na akina mama wa jamii ya kifugaji wamefurahia mpango huo na kusema kwamba utakuwa chachu kubwa ya kupiga hatua ya maendeleo, pamoja na kumaliza kabisa changamoto ya migogoro ya ardhi iliyokuwa ikijitokeza baina ya wafugaji na wakulima.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Jumuiko la Mali Asili Tanzania TNRF Bwana Zacharia Fustin amesema hatua ya serikali kuruhusu sera na sheria zitumike kutatua migogoro ya ardhi pamoja na kukabidhi hati miliki za Kimila kwa jamii ya kifugaji kutachagiza kumaliza migogoro ya rasilimali ardhi kwa wakulima na wafugaji.

Aidha, Mratibu wa Shirika la KINNAPA Bwana Abrahamu Akilimali amesema lengo la mpango huo ni yale maeneo yaliyokuwa yakihifadhiwa kiasili yaweze kufanyiwa umiliki wa kisheria ili kutunza na kulinda rasilimali ardhi na asili, pamoja na kumaliza migogoro ya ardhi.

Hati miliki za kimila 9 na vyeti vitatu vya usajili wa Ushirika wa wafugaji wa kuendeleza nyanda za Malisho;vimehusisha ukubwa wa eneo la ardhi kilomita 7,348 katika vijiji vya Kimbo;Allole na Napalai; ingawa Wilaya ya Kiteto ina ukubwa wa kilomita za mraba 16,875.
 Wa kwanza kushoto ni mkuu wa Wilaya ya Kiteto mkoani Manyara Bwana Tumaini Magesa akimkabidhi mwenyekiti wa kijiji cha Alole bwana Lamarai Nagwe hati miliki ya kimila sherehe iliofanyika katika kijiji cha Engang'oengare kilichopo Wilayani Kiteto Mkoani Manyara na kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali.
Mwenyekiti wa kijiji cha Alole Bwana Lamarai Nagwe, wa pili kushoto ni mkurugenzi wa Jumuiko la Maliasili Tanzania Bwana Zacharia Faustin, wa tatu kusho ni mkuu wa Wilaya ya Kiteto Bwana Tumaini Magesa pamoja na viongozi na wananchi kutoka katika vijiji vya Kimbo, Allole na Napalai wakiwa katika sherehe ya kukabidhiwa Hati miliki za Kimila na vyeti vya usajili wa Ushirika wa wafugaji wa kuendeleza nyanda za malisho zilizofanyika katika kijiji cha  Engang'oengare Wilayani Kiteto mkoani Manyara.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...