Na Said Mwishehe, Michuzi TV .
WAZIRI wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa Dk.Hussein Mwinyi amechukua fomu ya kugombea urais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibara kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM).
Dk.Mwinyi ambaye ni mtoto wa pili wa Rais mstaafu wa Serikali ya Awamu ya Pili Mzee Ali Hassan Mwinyi amechukua fomu hiyo leo Juni 17,mwaka 2020 katika ofisi za CCM Zanzibar huku akiomba radhi kwa waandishi wa habari baada ya kueleza kuwa hajajiandaa kuzungumza na vyombo vya habari kwasababu lengo lake ilikua ni kuchukua fomu ya kugombea urais tu.
Akizungumza baada ya kuchukua fomu hiyo Dk.Mwinyi amesema kuwa "Nianze kwa kumshukuru Mwenyezi Mungu kwa kutujaalia uzima na afya njema.Nimekuja kuchukua fomu ya kugombea urais wa Zanzibar.Pili nakishukuru Chama changu kwa demokrasi ya hali ya juu ndani ya chama inayomhusu kila mwanachama kugombea nafasi anayoitaka, hivyo nashukukuru kwa hilo.
"Niombe radhi leo sikuja kuzungumza na waandishi, nimekuja kuchukua fomu na tayari nimeshaichukua.Hivyo narudi kwenda kuangalia matakwa yanayotakiwa kwenye fomu hii ili niweze kuijaza na hatimaye nirudishe kabla ya muda kwisha.Mazungumzo yatakuwepo wakati mwingine, wakati muafaka, wala sina la kuzungumza maana hata yaliyoko kwenye fomu sijayajua, hivyo mtaniwia radhi, sitakuwa na mengi zaidi ya hayo,"amesema Dk.Mwinyi.
Kada wa Chama cha Mapinduzi ambaye pia ni Waziri wa Ulinzi na Jeshi la
Kujenga Taifa Dkt Hussein Mwinyi akionesha kwa Waandishi wa Habari (hawapo pichani) begi lenye fomu za kugombea nafasi ya Urais kwa Upande wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar
Katibu wa Oganaizesheni Zanzibar Garlo's Nyimbo akimkabidhi nyaraka mbalimbali
Kada wa Chama cha Mapinduzi ambaye pia ni Waziri wa Ulinzi na Jeshi la
Kujenga Taifa Dkt Hussein Mwinyi alipokwenda kuchukua fomu ya Kuomba
ridhaa ya kugombea Urais kwa Upande wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...