Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya
Mambo ya Ndani ya Nchi, Ramadhani Kailima, akitoa maelekezo ya Serikali
kwa Viongozi wa Chama cha Wafugaji Tanzania (CCWT) hawapo pichani, baada
ya kukuta Ofisi zao zikiwa zimefungwa na hakuna maandalizi ya Uchaguzi
Mkuu wa Chama hicho. Kailima, ameelekeza Wanachama wote wanaotaka
kushiriki kwenye Mkutano wa kuchagua Tume ya Uchaguzi utakaofanyika 25
Juni, 2020 wakalipe ada zao na kuwasilisha Stakabadhi katika Ofisi ya
Chama hicho. Taarifa hiyo ameitoa kwenye Mkutano na waandishi wa habari
uliofanyika leo jijini Dodoma.

Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya
Mambo ya Ndani ya Nchi, Ramadhani Kailima, akitoa maelekezo ya Serikali
kwa Viongozi wa Chama cha Wafugaji Tanzania (CCWT) hawapo pichani, baada
ya kukuta Ofisi zao zikiwa zimefungwa na hakuna maandalizi ya Uchaguzi
Mkuu wa Chama hicho. Kailima, ameelekeza Wanachama wote wanaotaka
kushiriki kwenye Mkutano Mkuu wa kuchagua Tume ya Uchaguzi utakaofanyika
25 Juni, 2020 wakalipe ada zao na kuwasilisha Stakabadhi katika Ofisi
ya Chama hicho. Taarifa hiyo ameitoa kwenye Mkutano na waandishi wa
habari uliofanyika leo jijini Dodoma.

Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya
Mambo ya Ndani ya Nchi, Ramadhani Kailima, akiwaonyesha waandishi wa
habari Ofisi za Viongozi wa Chama cha Wafugaji Tanzania (CCWT), ambazo
zilikuwa zimefungwa na hakuna maandalizi ya Uchaguzi Mkuu wa Chama
hicho. Kailima, ameagiza Viongozi wa Chama cha Wafugaji Tanzania waliopo
madarakani wahakikishe wanasimamia na kutekeleza Katiba yao na Sheria
ya Chama hicho. Taarifa hiyo ameitoa kwenye Mkutano na waandishi wa
habari uliofanyika leo jijini Dodoma.

Afisa Sheria Ofisi ya Msajili wa
Jumuiya za Kijamii wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Eliud Mwailafu
(Wa kwanza kushoto) akitoa taarifa ya Kamati inayoratibu Uchaguzi wa
Chama cha Wafugaji Tanzania (CCWT) kwa Naibu Katibu Mkuu wa Wizara hiyo,
Ramadhani Kailima (hayupo pichani) kuhusu mwenendo wa Maandalizi ya
Uchaguzi wa Chama hicho, jijini Dodoma. 

Mlango wa Ofisi ya Chama cha
Wafugaji Tanzania (CCWT) ambao ulikutwa umefungwa baada ya Naibu Katibu
Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Ramadhani Kailima na kamati
inayoratibu uchaguzi wa Chama hicho kutembelea ofisi hizo zilizopo Hotel
Fifty Six kuona mwenendo wa maandalizi ya Uchaguzi wa Chama hicho na
kukuta Ofisi hizo zikiwa hazijafunguliwa na Viongozi waliokuwepo
madarakani hawapo, leo 13 Juni, 2020 jijini Dodoma
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...