Charles James, Michuzi TV
MAELEKEZO yamefika! Ndivyo unavyoweza kusema baada ya Mkurugenzi wa Jiji la Dodoma kutangaza kuwa atafanya maamuzi ya kuoa kabla ya mwezi Desemba mwaka huu.
Ahadi hiyo ameitoa leo jijini Dodoma wakati akihojiwa katika kipindi cha Clouds 360 kinachorushwa na Televisheni ya Clouds ikiwa ni wiki moja tangu Rais Dk John Magufuli atoe wito kwake yeye na Mkuu wa Wilaya ya Dodoma wa kuwataka kuoa.
Akizungumzia suala la yeye kuoa, Kunambi amesema anafahamu kauli ya Rais Dk Magufuli ni ya Kiongozi wa Nchi lakini pia kama Baba hivyo ni muhimu kwake kutii.
Amesema sababu iliyopelekea kuchelewa kufanya maamuzi ya kuoa ni kutokana na kuwa ubize na majukumu ya kuwatumikia watanzania kiasi cha kukosa muda wa kufikiria wanawake.
" Kwa hakika nilipokea kauli ya Rais wetu kama kauli ya Kiongozi Mkuu wa Nchi na zaidi kama Baba. Rais alisema vile akiamini kijana wake nina uwezo wa kuanzisha familia na kuoa.
Hivyo niseme tu namuahidi kabla ya Disemba mwaka huu ntakua nimefanya maamuzi ya kuoa na harusi itafanyikia hapa hapa Dodoma, " Amesema Kunambi.
Rais Dk Magufuli akizindua jengo la Wakala wa Barabara Mjini na Vijijini (TARURA) jijini Dodoma wiki iliyopita alioneshwa kushangazwa kwake na kitendo cha Mkuu wa Wilaya ya Dodoma, Patrobas Katambi na Mkurugenzi wa Jiji hilo, Godwin Kunambi kutokua na Mke na kuwataka kuoa.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...