Uongozi wa
Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) unapenda kuutahadharisha Umma
kuwa waangalifu na wagonjwa wanaochangisha fedha kwa ajili ya kutibiwa
katika Taasisi hii. Ndugu Mwananchi, inawezekana wagonjwa hao
wanaochangisha fedha za matibabu wanakuwa tayari wamepata msamaha wa
matibabu kutoka kwa Taasisi au wasamaria wema wamewalipia.
Kama
utakutana na tangazo la aina hiyo kabla hujamsaidia mhusika tafadhali
wasiliana na uongozi wa Taasisi kupitia namba
0222152392/0782-042010/0688-027982 ili kupata ufafanuzi.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...